LISOME GAZETI LETU LA JAMHURI LA KILA WIKI HAPA

Habari Mpya

Yah: Uzalendo uliondoka kama Ujamaa na Kujitegemea?

Wanangu, leo nimeamka nikiwa na siha njema kabisa na kufurahi kwamba sasa mmeanza kuyaona yale ambayo labda sisi watu tunaoonekana wazee, mnaweza kuyaangalia kwa kina na kuyatafutia ufumbuzi wa kina ili tuondoke hapa tulipo twende huko kulikokuwa kunatarajiwa na wengi.

Read More »

Tujiepuke bejeti kiinimacho

Wiki hii Serikali inatarajiwa kuwasilisha bajeti bungeni mjini Dodoma. Bejeti hii inakisiwa kuwa ya wastani wa shilingi trilioni 15. Hili ni ongezeko la wastani wa trilioni 2 kutoka trilioni 13 za mwaka jana. Kiasi hiki ni kikubwa mno kwa takwimu. Kinawafanya Watanzania kuwa na matumaini makubwa ila yapo yanayotusikitisha.

Read More »

Kwa msimamo huu wa SMZ Muungano hauponi (1)

Mada hii ilitayarishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, na kuwasilishwa katika Mkutano Maalumu ulioandaliwa na Zanzibar Law Society Kuadhimisha Miaka 41 ya Muungano. Ulifanyika katika Hoteli ya Bwawani, Zanzibar mnamo Aprili 23, 2005. Ukisoma aya moja baada ya nyingine, utaona tofauti ndogo mno katika misimamo ya Uamsho na SMZ. Lililo wazi ni kwamba Muungano unakabiliwa na kifo. Endelea...

Read More »

Yai Sh. 900 hata mwendawazimu hakubali

Miongoni mwa mambo niliyoshindwa kuyaamini wakati wa vikao vya Kamati za Bunge vilivyofanyika Dar es Salaam wiki iliyopita, ni matumizi ya fedha za umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kuhusu bei ya mayai.

Read More »

Waziri Mukangara, Katibu Kamuhanda sema ukweli wote

Wiki iliyopita wahariri wa vyombo vyote vya habari nchini walikutana mjini Morogoro kujadili mustakabali wa tasnia ya habari nchini. Mkutano huo ulipaswa kufunguliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.  Waziri alikuwa na taarifa zaidi ya miezi miwili. Jumamosi ya wiki iliyopita ndipo akatuma ujumbe mfupi wa simu kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, akimweleza kuwa asingeweza kufika.

Read More »

Mabomu Mbagala siri zavuja

*Wakubwa walitumia (msiba huo) kutengeneza utajiri binafsi
*Ofisi ya Pinda yahaha kutafuta zaidi ya bilioni fidia mpya
*Waliopunjwa kucheka, hundi hewa milioni 260 zadoda

Miaka mitatu baada ya mabomu kulipuka katika Kambi ya Jeshi Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, siri nzito zimeanza kuvuja jinsi wakubwa walivyotumia msiba huo kujitengenezea utajiri binafsi.

Read More »

Jaji Warioba tunatarajia urejeshe Tanganyika yetu – 7

Wiki iliyopita nilichambua kwa kina kifungu cha 32 hadi 46A cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya madaraka ya Rais. Sitarejea niliyoyaandika lakini nashukuru kwa mrejesho mzuri wenye mshindo nilioupata. Wakati toleo hilo linatoka nilikuwa Lushoto mkoani Tanga, kwenye mafunzo yanayohusiana na masuala ya Katiba yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Read More »

Habari za Kitaifa

Maoni ya Mhariri

Nyundo ya Wiki