LISOME GAZETI LETU LA JAMHURI LA KILA WIKI HAPA

Habari Mpya

Jaji Warioba natarajia urejeshe Tanganyika yetu (3)

Katika ya pili ya makala haya nilieleza kuwa unaweza kuibuka uvivu wa kufikiri na baadhi ya watu wakahoji juu ya gharama za kuendesha serikali yenye ukubwa niliopendekeza. Kwa hiyo mimi napendekezo iwepo Serikali ya Tanganyika, ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Muungano.

Read More »

EWURA yazidi kubana wachakachuaji

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mafuta na Maji (EWURA) sasa imepiga hatua nyingine na kufanikiwa kudhibiti uchakachuaji wa mafuta ya dizeli na petroli, baada ya kuanza kutumia teknolojia ya vinasaba (maker).

Read More »

Bunge lamkaanga JK

*Kura ya kutokuwa na Imani ni kikombe cha shubiri
*Wabunge wanajipanga kupata kura 176 kumwadhibu
*Spika wa Bunge ameahirisha tatizo, Zitto aibuka shujaa

WIKI iliyomalizika ilikuwa ni ya msukosuko wa hali ya juu baada ya Bunge kuamua kumkaanga Rais Jakaya Kikwete kupitia mgongo wa mawaziri wake.

Read More »

Gari latengenezwa kwa Sh mil. 11, lauzwa kwa Sh mil. 1

Kwanza nimpongeze CAG pamoja na watu wa ofisi yake. Niwapongeze wenyeviti wote watatu kwa taarifa nzuri walizotusomea leo asubuhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naona suala hili ni kubwa na ni zito. Nadhani ni zito hata zaidi ya kupitisha bajeti. Kwa sababu bajeti tunapopitisha, ni fedha ambazo tunakisia tunadhani kwamba zitakusanywa. Hizi tunazozizungumzia leo ni fedha zimekusanywa zikaliwa - zimeliwa kwa njia nyingi.

Read More »

Serikali: Vitambulisho vya uraia vinatolewa bure

SERIKALI imewatoa hofu wananchi kwa kuwahakikishia kuwa vitambulisho vya uraia vitatolewa bure kwa Watanzania wote. Msimamo wa Serikali ulitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge.

Read More »

Habari za Kitaifa

Maoni ya Mhariri

Nyundo ya Wiki