LISOME GAZETI LETU LA JAMHURI LA KILA WIKI HAPA

Habari Mpya

Waislamu wachinje, sisi tule nguruwe wetu

Wiki iliyopita niliandika makala juu ya usaliti wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa yeye kuamua kuulisha umma uongo uliozaa madhara ya hali ya juu kwa wananchi wa Mtwara. Sitarudia nilichokiandika, ila niwashukuru wananchi na hasa wewe msomaji kwa mrejesho.

Nimepokea simu nyingi, ujumbe na barua pepe pengine kuliko wakati wowote tangu tuanzishe gazeti hili. Nawashukuru mno wasomaji kwa kueleza hisia zenu. Sitaweza kufafanua kila mmoja alisema nini, ila niseme karibu asilimia 95 ya waliowasiliana na mimi walinipongeza.

 

Sitanii, walinipongeza kwa kuamua kumfunga paka kengele. Hawakutarajia iwapo ningethubutu kumwambia Zitto kuwa katika hili hapana. Katika masuala ya nchi, siasa tuziweke kando. Alinichekesha msomaji mmoja aliyeniandikia hivi: “Kaka wengine wanatuchochea tupigane vita maana wanajua mambo yakiharibika kwetu watarudi kwao.”

 

Usiniulize ni nani mwenye uraia wa nchi mbili, ambaye hana uchungu na nchi yetu kiasi cha kutuchochea tupigane kisha arejee kwao. Ninalosema, gesi itunufaishe sote kama Watanzania. Nimemsikia Zitto ameanza tena uchochezi akidai Kigoma kuna mafuta, ila waelezwe watabaki na nini.


Sitanii, kichwa cha makala haya, kinasema: Waislamu wachinje, sisi tule nguruwe wetu. Nimelazimika kuandika makala haya baada ya kubaini sura ile ile ya upotoshaji katika jamii yetu. Mwanza kumeibuka kundi la watu wanaojiita Wakristo kuliko Waroma.

 

Kundi hili linashinikiza na kuhamasisha utengano katika jamii. Kundi hili limepeleka malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndekillo, likidai Wakristo waruhusiwe kuchinja. Waziri wa Uhusiano wa Jamii, Stephen Wasira, amefika pale akajaribu kusuluhisha mgogoro huu, inaelekea ameshindwa.

 

Nikisoma katika mitandao naona wakubwa huko Mwanza wameanzisha hadi bucha zao. Wanachinja wenyewe na kuwauzia Wakristo wenzao. Nimejaribu kufuatilia chimbuko la mgogoro huu. Wanasema Waislamu wanawadharau kwa kula nguruwe.


Eti Waislamu wanataka hata maduka ya nguruwe yaliyopo katika mitaa yao yavunjwe kuepusha kukwaza imani yao. Hapo ndipo ninapopingana na Waislamu sawa na nilivyopingana na Wakristo. Katika utawala wa Awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi, nchi yetu ilipata mgogoro kama huu.  Mzee Mwinyi alimaliza tatizo hili kwa busara ya hali ya juu.

Read More »

JAMHURI yaisafisha TTCL

Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imemng’oa katika madaraka Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Said Amir, na kuwasimamisha kazi maofisa wengine watatu waandamizi ili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi zinazowakabili.

Read More »

Mangula kazima moto kwa petroli Bukoba

Kwa karibu miezi sita sasa, siasa za Jimbo la Bukoba mjini zimegeuzwa siasa za chuki, kutishana, fitina, kuchambana, kulaumiana, kuonesha umwambwa, uwezo wa kifedha, dharau, ubaguzi  na ujenzi wa matabaka yanayosigana katika jimbo hili.

Read More »

Kagasheki atiwa majaribuni

Kundi la wafanyabiashara kadhaa wa tasnia ya uwindaji wa kitalii, limekutana nchini Marekani na kuendesha mchango wa mabilioni ya shilingi kufanikisha ugawaji upya wa vitalu vya uwindaji.

Read More »

Vinara mgogoro wa gesi watajwa

Matajiri wakubwa nchini wanaojihusisha na biashara ya mafuta ya petroli, mafuta mazito ya viwandani na kampuni kubwa za kimataifa, ni miongoni mwa wanaochochea mgogoro wa kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam , JAMHURI imethibitishiwa.

Read More »

NUKUU ZA WIKI

Nyerere: Nilipata ajali ya kihistoria

“Kitaaluma mimi ni mwalimu wa kufundisha darasani; lakini kwa sababu ya ajali ya kihistoria nilijikuta nikiwa kiongozi wa mapambano ya kudai uhuru na baadaye kiongozi wa nchi yetu.”

 

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Read More »

RATIBA YA AFCON 2013

Jumanne 29 Januari, 2013 Ethiopia vs Nigeria            saa 3:00 usiku Burkina Faso vs Zambia    saa 3:00 usiku Jumatano 30 ...

Read More »

Habari za Kitaifa

Maoni ya Mhariri

Nyundo ya Wiki