LISOME GAZETI LETU LA JAMHURI LA KILA WIKI HAPA

Habari Mpya

Mrina Annex: Kivuli cha wakware Arusha

Si mara yangu ya kwanza kufika Arusha, lakini hii ni safari yangu ya kwanza kuzuru Arusha ikiwa “imepachikwa” hadhi ya kuitwa jiji. Kwangu mimi, Arusha ni “zizi.” Kama wingi wa watu ndiyo kigezo pekee cha mji kupandishwa hadhi na kuitwa jiji, basi watawala wetu watakuwa wanakosea.

Read More »

Hatari mpaka wa Sirari

*Biashara ya magendo yafanywa nje nje

*Maofisa wa TRA, polisi wahusishwa

*RPC, Meneja TRA wakiri hali mbaya

Biashara ya magendo imeshamiri katika mji wa Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya, huku vyombo vya dola vikionekana ama kushindwa au kushirikiana na madalali maarufu kwa jina la “mabroka”. Vitendo hivyo vinaendelea kuikosesha Serikali mapato kutokana na bidhaa nyingi kuingizwa Tanzania na hata kupelekwa Kenya kupitia “njia za panya” bila kulipiwa kodi na ushuru.

Read More »

NUKUU ZA WIKI

Nyerere: Tuchague viongozi wanaostahili

“Ni dhahiri kwamba uongozi wa Chama chetu lazima ushikwe na wanachama wa CCM. Tunachoweza kukosolewa ni kwamba wakati mwingine tunachagua viongozi wasiostahili.”


Haya yalisemwa na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akihimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuondokana na kasumba ya kuchagua viongozi wasiostahili.

Read More »

Yah: Kama ningekuwa waziri wa dawa na matibabu…

Wanangu, poleni na kazi na hongera sana kwa kuvuka mwaka 2012. Nasikia mnapeana “Happy New Year” kila ninakopita na mnashangilia kwa nguvu, sina hakika mnashangilia kwa sababu zipi, lakini nafikiri kuumaliza mwaka siku hizi ni kazi ya ziada kutokana na maradhi na misukosuko mingi ya maisha.

Read More »

Muungano ndiyo mboni ya Tanzania (4)

Vyama vikubwa Visiwani vilikuwa ARAB ASSOCIATION, INDIAN ASSOCIATION na AFRICAN ASSOCIATION. Na kutokana na vyama hivyo, vikajazaliwa vyama kama SHIRAZI ASSOCIATION na UMMA PARTY.

Read More »

Mwaka 2013 uboreshe michezo Tanzania

Tangu mwaka 1974 wakati Filbert Bayi alipoweka rekodi mpya ya mita 1,500 duniani, Tanzania haijapata mafanikio mengine makubwa kiasi hicho katika riadha na hata michezo mingineyo.

Read More »

Mwaka mpya tuchape kazi

 

 

 

Leo ni Mwaka Mpya. Ni mwaka 2013. Tunafahamu Januari hii ni kichomi kwa familia nyingi. Iwe kwa matajiri au masikini, waajiri au waajiriwa ni mwezi wa tabu. Kodi za nyumba zinadai, ada za shule zinadai, wenye magari mengi yanaisha bima na hati za njia na hata wenye kununua viatu na nguo kwa msimu zimekwisha, wanahitaji vipya.

Read More »

Nawaunga mkono wananchi wa Mtwara

 

Niliposikia kwamba wananchi wa Mtwara wameandaa maandamano kupinga usafirishaji gesi kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam, sikuamini. Kutoamini kwangu kulitokana na dhana iliyojengeka kwa miaka mingi kwamba wakazi wa mikoa ya kusini si “wakorofi” kama walivyo ndugu zao wa mikoa kama Mara, Kilimanjaro au Arusha.

Read More »

Ujue uhalifu ulioiandama Tanzania 2012

Mwaka 2012 utakumbukwa pamoja na mambo mengine nchini, kwa matishio kadhaa yakiwamo ya uharamia baharini, wahamiaji haramu, biashara haramu ya usafirishaji binadamu, ajali za barabarani, biashara ya dawa za kulevya, uingizwaji wa silaha haramu, bidhaa bandia, uhalifu dhidi ya mazingira na maliasili.

Read More »

Habari za Kitaifa

Maoni ya Mhariri

Nyundo ya Wiki