Rais Dkt. John Pombe Magufuli amevitaka vyombo vya dola kuwatafuta na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika waliohujumu kiasi cha shilingi bilioni 2 katika mradi wa maji wa Ntomoko ulioko wilayani Kondoa.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana wilayani Kondoa alipokuwa akifungua Barabara ya Dodoma hadi Babati yenye kilomita 251.

“Wahusika watafutwe ili warudishe fedha walizochukua au wahakikishe mradi unakamilika. Ni lazima watu waogope mali ya watu masikini,” alisema Rais Magufuli.

Ameendelea kwa kusema, kama viongozi wanawajibu wa kuchukua hatua hata kama zinauma lakini ni kwa manufaa ya Watanzania milioni 55.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka wananchi wa wilaya ya Kondoa kuitunza miundo mbinu ya barabara ambayo ameizindua. Aidha amesema wapo Wananchi ambao wamekuwa wakiondoa alama za barabarani na kwenda kutengenezea tela za ng’ombe au kujengea vyoo.

By Jamhuri