Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamuapisha Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamuapisha Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Januari 8, 2018, asubuhi.

Biteko akila kiapo.

 

Baada ya kuapishwa, Mhe. Dotto Biteko amesema;

“Kwanza namshukuru Mungu  kwa siku ya leo na namshukuru kwa kuweza kutokea haya yote. Nakushukuru wewe Mheshimiwa rais kwa kuweza kuniteua, sina la kukupa ila kutenda kazi kwa bidii. Mhe. Rais nina bahati kubwa sana na hata wewe umelishuhudia kwenye mikutano mingi sana, umenipa sifa kubwa kwa kuhudumu chini ya mwanamke ambaye ni mchapa kazi sana. Niko tayari kufanya kazi kwa bidii na namuomba Mungu usije jutia uamuzi wako,” alisema Biteko.

Naye Mhe. Spika Ndugai alipota fursa ya kuzungumza akasema;
“Sisi Bunge tumekuwa tukishauri kwa muda sana kwa serikali kuwa wizara ya nishati na madini imekuwa wizara kubwa na nzito sana na nashukuru umeifanyia kazi kwa kuweka wizara mbili za madini na nishati. Tunakushukuru sana mheshimiwa Rais. Mhe. Dotto ni mchapakazi na ana utumishi uliotukuka,” alisema Ndugai.

 

1702 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!