SMZ imeibiwa mabilioni

 

576. Benki Kuu yaTanzania ibuni mbinu za kupunguza matumizi ya fedha taslim katika uchumi wetu. Sheria zote muhimu zifanyiwe marekebisho ili kuwabana wale wote wanaolimbikiza fedha majumbani mwao.

 

577. Kampuni au biashara inaposajiliwa, wanaohusika na kusajili watoe taarifa kwa Mamlaka ya Mapato mara moja. Mwenye biashara au kampuni kama hajachukua leseni kwa kipindi cha mwaka mmoja aingizwe kwenye orodha ya walipa kodi.

 

578. (i) Mamlaka ya Mapato iwe na ofisi za malalamiko dhidi ya utozaji kodi holela, ukwepaji kodi kwa washindani na kwa maafisa ambao watawatendea wateja vibaya.

 

(ii)Mamlaka ya Mapato iwe na ofisi au kamati za kusikiliza rufani za walipakodi. Rufani hizo zisikilizwe ndani ya siku 14 baada ya kuwasilisha rufani na pasiwepo na haja ya kulipa sehemu yoyote ya kodi kabla ya rufani kusikilizwa atakayeomba rufani atakiwe kulipa ada ya kukata rufani.

 

579. Tume ya Mtei pamoja na Tume ya Mramba zimependekeza utozaji kodi kwa majengo yanayopangishwa katika miji. Misingi ya utozaji kodi hii uwe ni thamani ya jengo. Tume inaafiki kwamba ni vizuri  mapendekezo hayo yakatekelezwa sasa ili kuboresha makusanyo ya mapato ya Serikali.

 

600. (i) Serikali iandae utaratibu utakaotumika kuwatoza  wakulima na wafugaji kodi ya mapato ili kupanua wigo wa kodi ya mapato.

 

(ii)Serikali ibuni mfumo wa kuwapatia maskani maalum ya biashara wale wote wanaofanya biashara barabarani na barazani bila ya leseni.

 

(i)                Halmashauri za jiji, miji na wilaya zibuni mbinu za kuwatoza watembezaji bidhaa ada ya leseni za biashara ili kujenga utamaduni wa kufanya biashara kulingana na sheria.

 

(ii)             Serikali za mitaa zihamasishe Serikali za vijiji kukusanya Kodi ya Maendeleo kwa kuziachia asilimia ya mapato yatakyaokusanywa na vijiji hivyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

 

KIAMBATISHO A

 

MAKUSANYO YA KODI KWA KIPINDI CHA 1990/91 – 1994/95

 

 

1990/91

1991/92

1992/93

1993/94

1994/95

Total Revenue

137,092.9

173,565.5

164,109.9

237,897.0

311,280.0

Tax Revenue

118,257.8

153,355.6

146.419.0

221,258.0

270,940.0

Customs & Excise

56,319.9

51,638.6

36,706.0

57,819.0

81,318.0

Income Tax

32,413.0

40,143.0

45,455.0

63,026.0

86,684.0

Sales Tax

20,171.6

44,862.2

41,047.0

57,578.0

72,645.0

Others Taxes

9,353.3

16,711.8

23,211.0

42,835.0

39,293.0

 

 

KIAMBATISHO B

 

WAKALA WA FORODHA WALIOFUNGIWA LESENI KUTOKANA NA MATUMIZI YA HATI BANDIA KUTOA MAKASHA (CONTAINERS) MANANE AMBAYO YALIKAMATWA

KAMPUNI

WAKURUGENZI

SABABU

1.     TARU (R ) RUSUA Co.

Box 46626

DSM

Yisambi Robert Mboma

Shali Robert Mboma

Yisega Yisambi Nicodemus

Kukwepa Ushuru wa Forodha kwa kutumia hati bandia kuondoa mali bandarini

Ushuru – Shs.18,522,845/-

Sales Tax Shs. 12,920,729/-

2.     Marik Freight

Box 4614

DSM

Josephat J. Mwakitwange

Ramesh Jayantilal Patwa

Kukwepa Ushuru wa Forodha kwa kutumia hati bandia

Ushuru: Shs. 26,597,935/-

Sales Tax: Shs. 13,805,747/-

3.     Truck Freight

Box 16552

DSM

Jamal A. Ahmed

Abdallah A. Ahmed

Kukwepa kodi kwa kutumia hati bandia Ushuru: Shs. 7,627,190/-

 

KIAMBATISHO C

 

SUMMARY OF QUANTITIES OF PETROLEUM PRODUCTS DUMPING FOR THE PERIOD OF JUNE 1994 TO 1995

 

 

Company

MSP

(lts.)

JET A-1 (lts.)

IK

(lts.)

GO (lts.)

FO (lts.)

SUM

 (lts.)

AGIP

 

DP-DSM

 

BP-MBEYA

 

BULKOIL

 

GAPCO

 

CALTEX

 

MOBIL

 

TOTAL (T)

 

2,779,203

 

14,922,743

 

 

 

6,996,524

 

 

1,716,014

 

 

1,876,091

 

10,639,093

 

7,376,466

 

 

 

 

141,208

 

5,573,255

 

 

 

44,645

 

2,040,983

 

 

757,000

 

57,443

741,542

 

94,174

 

46,454

 

 

185,763

 

274,433

 

1,648,111

7,070,397

 

16,451,766

 

 

 

5,923,661

 

1,605,730

 

327,733

 

4,690,524

 

11,874,085

 

12,374,085

72,832

 

 

100,330

 

 

 

 

50,245

10,805,182

 

37,041,908

 

12,920,135

 

3,513,673

 

2,368,766

 

6,752,378

 

23,444,611

 

22,006,413

SUM

46,306,134

8,614,504

2,990,477

60,718,099

233,907

118,353,121

 

 

AMOUNT INVOLVED AS PER PRICE STRUCTURE

 

 

 

MSP (Tshs.)

JET A-1 (Tshs.)

IK

(Tshs.)

GO (Tshs.)

FO (Tshs.)

SUM (Tshs.)

T.E.F.

P.S.R.F.

80,072,567

3,510,704

5,171,133

104,993,737

611,067

214,359,228

Sales Tax

23,153,067

8,614,504

1,495,239

30,359,050

223,907

63,845,766

Ex. Duty

1,774,932,639

53,937,132

18,798,737

0

1,478,615

1,849,147,123

F.O.B. Diff.

470,403,178

9,184,374

 

75,253,290

26,060,061

435,785,940

 

435,785,940

2,521,517

 

1,955,973

1,003,955,670

 

965,290,973

Road Toll

427,667,246

 

1,736,480,025

0

24,683,522

 

0

283,928,713

 

4,013,408,738

 

4,512,708,722

230,500,006

76,154,294

3,283,853,379

6,791,099

8,110,007,497

 

T.E.F = Transport Equalization Fund; P.S.R.F= Petrol Sector Rehabilitation Fund

 

 

KIAMBATISHO D

 

MIFANO YA WAKALA WA MIZIGO WALIOFUNGIWA LESENI KWA KUSHINDWA KUTOA TAARIFA KUHUSU USAFIRISHAJI WA TRANSIT GOODS

 

 

KAMPUNI

WAKURUGENZI

SABABU

1. Jambo Freight

P.O. Box 4614 DSM

G. Mahinda,

 J. Mzuanda

Kushindwa kuwasilisha taarifa za kuonyesha kama mali waliyokuwa wapeleke Transit imepelekwa inakohitajika Ushuru – Revenue Liability BIF Shs. 12,620,374/-

2.Oriental C & F

P.O. Box 71305 DSM

Mrs. Hamida Thabit

Ali Senyange

Kushindwa kutoa taarifa kama mali iliyokuwa isafirishwe kwenda nchi jirani imefika inakohitajika – Ushuru Shs. 622,872,542/-

1.     Trans Ocean (Uganda Ltd), P.O Box 9770 DSM

Mr. Kagwa

E. Okuraja

Kushindwa kuwasilisha taarifa kama mali waliyokuwa wapeleke nchi jirani imefika inakohitajiwa. Ushuru – Revenue Liability Shs. 268,301,536/-

2.     Chanya Investment

P.O. Box 60672 DSM

Donald Chacha

F. Oluoch Nyarara

-do-

Revenue Liability Shs. 56,036,256

3.     Overseas Trade Ways

P.O. Box 70489 DSM

Andrew Kagwa

Bigirimfura A.

E. hakizimfura

-do- Revenue Liability Shs. 10,701,268/-

4.     Inter Africa C & F Dar es Salaam

Godfrey Sindani

Charles Nkuba

Aron Nkuba

-do-

 Revenue Liability Shs. 12,620,374/-

5.     Agree Group Agencies

Hashim Rungwe

 

Revenue Liability Shs. 392,000,000/-

 

 

KIAMBATISHO E

 

Hill Top Hotel and Tours Ltd inayomilikiwa na Mohsin Abdallah na Hitesh P. Arjun ilipewa Certificate of Approval Enterprise na Kituo cha Uwekezaji Rasilimali tarehe 3/1/1991. Baadaye watu hoa walianzisha kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel iliyosajiliwa tarehe 2/4/1992 na ambayo ilirithi ‘Certificate of Approval Enterprise iliyokuwa imetolewa kwa kampuni ya Hill Top Hotel and Tours kuendeleza ujenzi wa Hotel ya Kitalii ya Kigoma. Kampuni hii mpya inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Hitesh Arjun na Deusidedit Kisisiwe. Wamiliki hawa pia wanamiliki makampuni mengine ama kwa pamoja au mmoja wa kama ifuatavyo.

 

(i)                SHENIS COMMERCIAL LTD, inayoshughulika na mauzo ya nguo, vitambaa na vipuri vya magari na mashine inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Mrs. Nargis Mohsin Abdallah na Deusdedit Kisisiwe. Kampuni hii ilisajiliwa tarehe 27/7/1988.

 

(ii)             TILE AND TUB LTD iliyosajiliwa tarehe 7/12/1992 inashughulikia na biashara ya vifaa vya ujenzi, umeme, pombe na madawa na inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Deusidedit Kisisiwe na Tariq Mirza.

 

(iii)           FIVE WAYS CLEARING AND FORWARDING AGENCY iliyosajiliwa tarehe 23/10/1992 kwa ajili ya kuondoa mizigo bandarini na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa njia mbalimbali biashara ya vipuri na vifaa vya ujenzi uchimbaji na uuzaji wa madini nchi za nje inamilikiwa na Triphon Maji na Deusdedit Kisisiwe.

 

(iv)           ROYAL FRONTIER (T) LTD iliyosajiliwa tarehe 7/3/1994 kwa ajili ya uwindaji wa kitalii na usafirishaji wa watalii inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Deusidedit Kisisiwe na Rashid Omar.

 

(v)             GAME FRONTER (T) LTD na MNM Hunting Safaris Ltd inafanya shughuli zinazofanana na zile za Royal Frontier na inamilikiwa na Mr. Mohsin Abdallah, Mr. Abdikadir Mohamed na Mr. Ahmad Muhidin.

 

Shenis Commercial Ltd ndiyo kampuni ya kwanza kisha ikafuatiliwa na Kigoma Hill Top. Baadaye makampuni mengine yaliibuka haraka haraka jambo linaloashiria kwamba yalitokana na Kigoma Hill Top na yanafanya shughuli zake kwa kushirikiana.

 

Vifaa vilivyoagizwa na Kigoma Hill Top na kusamehewa kodi ni vingi kuliko mahitaji ya hoteli kwa mfano kampuni iliagiza vigae vya sakafu 27,248, containers 3 za marumaru zenye ujzao wa mita za mraba 3264.8, magodoro 120 na taulo 4000 wakati hoteli ina vitanda 60 tu.

Aidha iliruhusiwa kuagiza boti tatu na injini nne (outboard engines) na kufanya Hotel huyo kuwa na boti 7. Idadi hii ya boti ambazo imeelezwa kwamba zitatumika kwa uvuvi wa kitalii ni nyingi sana ikilinganishwa na idadi ya vyumba vya Hotel hiyo inawezekana zitatumiwa kwa shughuli nyingine. Vifaa vya ziada inaaminiwa viliuzwa na makampuni mengine yanayomilikiwa na wakurugenzi wa Kigoma Hill Top Hotel.

 

Taarifa ya IPC inaonyesha kwamba ingawa kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel ilipatiwa misamaha ya kodi. IPC haikuona na kupendekeza aina ya vifaa vya ujenzi wa Kigoma Hill Top Hotel vinavyotakiwa kusamehewa kodi. Wakurugenzi wa kampuni walikuwa wanawasiliana na Hazina moja kwa moja kuanzia mwaka 1991 hadi Julai 1995 walipoanza kupitisha maombi ya misamaha hiyo IPC.

 

Hata hivyo baadhi ya vifaa ambavyo vilisamehewa kodi na Hazina havikusastahili kusamehewa kodi. Kwa mfano kampuni ilisamehewa kodi Magari Na. TZF 5059 Toyota S/Wagon, TZF 8455 Toyota L/Cruiser, TZF 8612 Landcruiser S/Wagon na TZF 6001 ambalo ni gari ya kifahari ya aina ya Mercdes Benz Sportscar, na ndege moja.

 

Ijapokuwa  magari na ndege hiyo vyote vilisamehewa kodi chini ya mradi wa Kigoma Hill Top yamekuwa yanatumika na kampuni zao nyingine hapa Dar es Salaam na Kigoma. Kwa mfano gari Na. TZF 8454 lililoandikishwa tarehe 16/6/1994 kama mali ya Kigoma Hill Top, chini ya Import Declaration mwagizaji alikuwa Royal Frontier na Import Entries zilionyesha Kigoma Hill Top.

 

Kampuni hii ilikuwa iagize ndege mwaka 1995 na ikasemehewa kodi kwa barua Kumb. Na TYC/1/150/9/176/7. Uchunguzi umeonyesha kwamba hakuna ndege iliyosajiliwa hapa nchini kwa jina la kampuni hiyo lakini kampuni ya Game Frontiers ina ndege yenye namba za Usajili 5H-GFT (Cesna 206) iliyosajiliwa mwaka 1995.

 

Uchunguzi pia unaonyesha kwamba kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel inatumia sana ndege hiyo kwa kuwapeleka watalii na wageni huko Kigoma Hill Top Hotel ingawa haina leseni ya biashara ya usafiri wa anga. Ifuatayo ni taarifa ya Idara ya Forodha kuhusu misamaha ya Kodi iliyotolewa na Hazina kwa ajili ya Magari, marumaru, sanitary ware na vifaa vya umeme.

 

 

Kifaa

Kibali cha Hazina

CIF Value

Import Duty

Sales Tax

Jumla ya misamaha

Tan 389

Jan 94

1 Toyota L/cruiser

TYC/1/150/9/176/9 of 20/9/93

24,493,406.81

9,796,960.73

13,372,852.94

23,269,813.67

Tan 515 Jan 1994 1 Toyota L/Cruiser

-do-

26,515,578.58

5,303,334.12

7,995,001.17

13,258,335.29

Tan 398 of March 94 I M/Benz

-do-

42,075,345.09

16,840,138.04

22,973,138.42

39,813,276.46

Tan 202 of Feb 1994  Sanitary ware

TYC/1/150/9/176/7 of 9/7/93

9,927,493.38

2,678,250.58

3,481,723.25

6,159,973.38

Tan 18 of Dec. 1993 Ceramic tiles

-do-

11,702,352.83

3,510,707.22

4,563,918.02

8,074,625.24

Tan 1305 of Aug. 1993 Lighting Fixtures

-do-

7,194,846.44

2,158,451.85

2,805,995.68

4,964,447.53

 

JUMLA

 

 

40,287,842.54

55,152,629.48

95,440,472.02

 Tume imezungumza na mmoja wa wamilikaji wa kampuni ya Kigoma Hill Top Bw. Deudedit Kisisiwe lakini maelezo aliyoyatoa kuhusu tuhuma hizo hayakuridhisha. Tume inaamini kwamba;

 

(i)                Bwana Mohsin Abdallah na wenzake, hasa Deusdedit Kisisiwe wamefungua kampuni nyingi za biashara na kuomba misamaha ya kodi kwa kampuni moja ya Kigoma Hill Top Hotel Kampuni imeagiza vitu vingine vilivyosamehewa kodi na kuvitumia au kuviuza kupitia makampuni yao mengine ambayo hayakupata misamaha ya kodi.

 

(ii)             Wafanyabiashara wamekuwa wanawatumia viongozi wa Serikali katika kuficha maovu yao. Kwa mfano Kampuni ya Fiveways Clearing and Forwarding Agency ilimpa hisa Bw. Tryphon Maji aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es salaam na hivyo alikuwa habughudhiwi na Polisi anapofanya vitendo kinyume na kanuni na taratibu.

 

Katika kampuni ya Royal Frontier (T) Ltd hisa zimetolewa kwa Ahmed Muhidin ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori Bw. Muhidin Ndolanga. Hisa hizi zimetolewa kwa wakubwa hawa kama vivuli (cover) ili waweze  kuyapatia makampuni haya vitalu vya Uwindaji pamoja na kurahisisha shughuli za Uwindaji.

 

(iii)           Bw. Mohsin Abdallah na Kisisiwe wanapenda kuwatumia viongozi kama chambo katika biashara zao ili waweze kuvuka kikwazo chochote kile kitakachokwamisha biashara zao.

 

KIAMBATISHO F

 

MUHTASARI WA KODI YA ZIADA ILIYOKADIRIWA NA KUKUSANYWA NA IDARA YA FORODHA BAADA YA TANS KUTOLEWA NA SGS NA INCHCAPE

KIPINDI

MAKUSANYO

Mwaka wa Fedha 1994/95

Shs. 908,306,784.00

Mei 1995

Shs. 218,098,558.00

Juni 1995

Shs. 128,092,558.00

Julai 1995

Shs. 70,761,300.00

Agosti 1995

Shs. 165,367,620.00

September 1995

Shs. 86,897,504.00

Oktoba 1995

Shs.125,494,275.00

Novemba 1995

Shs. 128,977,294.00

Desemba 1995

Shs. 70,397,848.00

Januari 1996

Shs. 729,252,949.00

 

JUMLA

 

Shs. 2,285,459,533.00

 

 

 

KIAMBATISHO G

 

REVENUE RECONCILIATION SUMMARY SERVICES OF INCHCAPE OCTOBER 1995 TO FEBRUARY 1996

 

 

Month

Duties and taxes assessed

Value of exemptions

Duties and taxes payable

Total collections

% of 5 to 4

1

2

3

4

5

6

Oct. 1995

5,218,726.1

2,560,640.7

 

1,808,312.0

2,658,085.4

 

2,515,790.0

1,119,381.8

 

1,112,887.0

42

 

44

Nov. 1995

4,324,102.0

 

1,359,593.0

1,479,202.0

1,084,608.0

73

Dec. 1995

2,838,795.0

 

2,355,761.5

2,668,637.2

1,175,929.8

44

Jan. 1996

4,024,398.7

 

7,084,307.2

9,321,714.6

4,492,806.6

48

 

TOTAL

 

 

16,406,021.8

 

 

 

 

 

Chanzo: Inchcape Testing Services – Pre-shipment Inspection Monthly Reports – October 1995 – February 1996.

 

KIAMBATISHO H

 

WIZI WA USD 434,716.23 KATIKA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR

 

Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar Bw.  Naushad Mohamed Suleiman alikuwa na A/C ya fedha za kigeni katika Benki ya Wananchi wa Zanzibar. Katika kipindi cha tarehe 13 Julai 1991 mpaka Februari,1992 aliweza katika nyakati mbali mbali kutoa jumla ya USD 434,716.23 bila fedha hizo kuingizwa kwenye akaunti yake na hivyo kupelekea akaunti yake kuwa ‘overdrawn.’

 

Benki ilichukua hatua za kumshawishi mteja kusawazisha madeniyake na alikataa. Bodi ya PBZ iliamua kumshtaki na ikawasilisha shauri hilo Polisi kwa upelelezi wa kina na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Upelelezi wa kesi hii ulifanyika kwa pole pole sana baadaye Polisi wakaeleza kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kumshataki mfanyabiashara huyu.

 

Hata hivyo, PBZ ilieleza kwamba yenyewe ina ushahidi tosha wa kuweza kufungua kesi ya madai dhidi ya mteja huyu. PBZ ilifungua kesi ya Madai Na. 13 ya mwaka 1995. Baada ya kufunguliwa kwa kesi hiyo Serikali ya Mapinduzi ilitoa shinikizo na kwa barua ya Wizara ya Fedha ya Februari 15, 1996 Benki iliagizwa kufuta kesi hiyo na kutafuta njia nyingine kufidia hasara iliyopatikana.

 

Tume ilifanya uchunguzi wa suala hili ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wajumbe wa Bodi ya PBZ na maoni ya Tume ni kwamba haikuwa sahihi kwa Serikali kuingilia suala hili lisifikishwe mahakamani.

 

Je, unafahamu Jaji Warioba katika ripoti hii aliyoiandaa mwaka 1996 alipendekeza ni kuhusu eneo la ardhi? Ingawa ripoti hii imeandikwa mwaka 1996, inaendelea kuwa na maudhui yenye uhalisia na yenye kuonyesha upungufu ule ule hadi sasa na hivyo inastahili kufanyiwa kazi. Usikose JAMHURI wiki ijayo. Mhariri.

1413 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!