Timu ya Simba wamerejea jijini Dar es Salaam leo wakitokea Morogoro.

Simba wamerejea jijini Dar es Salaam wakitokea Morogoro, hali ambayo imewashangaza wengi.

Kawaida huondoka siku moja kabla ya mechi, lakini Simba wameamua kurejea Dar es Salaam siku mbili kabla.

Simba ilikuwa Morogoro kujiandaa na mechi dhidi ya watani wake Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

Yanga pia wameweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

1889 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!