Uwanja wa ndege za kivita wa Syria washambuliwa kwa makombora
Watu kadha wamefariki katika uwanja mmoja wa ndege wa kijeshi nchini Syria baada ya shambulio la kutumia makombora, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vinasema. Shirika la serikali la SANA limesema makombora kadha yalirushwa uwanja wa ndege wa Tayfur, ambao pia hufahamika kama T4 karibu na mji wa Homs, mapema leo Jumatatu. Maelezo zaidi…