MWALIMU NANI? ADHA ZA TAKSI DAR ES SALAAM
Mapema mwezi huu nikiwa Dar es Salaam nilituma ujumbe kuomba huduma ya usafiri wa Uber, huduma nafuu ya usafiri wa taksi ambayo imeleta nafuu ya gharama za usafiri jijini humo. Katika kutumia Uber nimegundua tatizo moja la msingi. Madereva hawana uzoefu wa kutosha wa kusoma ramani kubaini mteja yuko wapi. Kwa sababu hiyo, wanalazimika kupiga…