Saba Wafariki kwa kipindupindu Rukwa.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amethibitisha kufariki kwa wagonjwa saba wa kipindupindu katika Wilaya ya Sumbawanga huku wagonjwa wengine 44 wakibaki wodini kuendelea kupatiwa matibabu na wagonjwa 115 wakiruhusiwa kurudi nyumbani. Amesema kuwa ugonjwa huo umelipuka tarehe 6 Mei, 2018 katika Kijiji cha Mayenje, kata ya Milepa katika bonde la ziwa Rukwa…