Telegramu yaitupia lawama Apple kwa kuicheleweshea huduma

Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Telegram, Pavel Durov, ameikaishifu Apple kutokana na mchakato wa kampuni hiyo wa kukagua duka la Programu (Apple Store) “usio wazi” ambao unaichelewesha Telegram kutoa sasisho (ku-“Update”) kwa programu yake ambayo “itabadilisha jinsi watu wanavyojieleza katika kutuma ujumbe.”

Picha ya chapisho la Mkurugenzi Mtendaji wa Telegraph Pavel Durov akikosoa mfano wa duka la programu

Kupitia idhaa yake katika mtandao wa Telegram Durov amesema kwamba sasisho (updates) la Telegram katika iOS ambalo linatarajiwa kubadilisha jinsi watu wanavyowasiliana limekwama katika mchakato wa ukaguzi wa duka la program la Apple (Apple Store) kwa zaidi ya wiki mbili sasa bila mawasiliano kutoka kwa kampuni hiyo juu ya kwanini au lini itaidhinishwa

Durov anadokeza kwamba ikiwa program maarufu kama Telegram inapokea huduma ya namna hiyo kutoka kampuni ya Apple basi anaweza kufikiria matatizo na changamoto zinazowakumba watengenezaje wa progamu ndogo Zaidi.

“Unaweza kufikiria matatizo yanayokumba wasanidi programu wadogo zaidi.
Kwa mfano,sasisho (update) letu lijalo ambalo linakaribia kuleta mapinduzi ya jinsi watu wanavyojieleza katika utumaji ujumbe limekwama katika ukaguzi wa Apple kwa wiki mbili sasa, bila maelezo au maoni yoyote kutoka Appl.” amesema Durov

Hata hivyo haijulikani mpaka sasa ni kwa nini Apple inachelewesha sasisho la program ya Telegram ili kuwafikia mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo.

Kwa kawaida programu nyingi hukaguliwa kwa haraka sana na kuidhinishwa na hivyo tukio hili la Apple linazua hisia tofaui juu ya mtandao wa Telegram

Kupitia tovuti yake Apple inasema “kila wiki zaidi ya wataalamu 500 waliojitolea duniani kote hukagua zaidi ya program laki moja na zaidi ya mawasilisho milioni moja hukataliwa”

Durov alijadili hali hiyo isiyoelezeka kama sehemu ya ukosoaji mpana wa miundo ya bishara ya duka la program (Apple Store), hata hivyo si mara yake ya kwanza kuwakoromea Apple. Mnamo mwaka 2018 pia amesema kuwa Apple imekuwa ikizuia sasisho la program za Telegram ndani ya iOS, mara baada ya Urusi kuipiga marufuku Telegram na baada ya siku moja iliidhinishiwa sasisho.

Telegram ni programu inayowawezesha watumiaji kutuma ujumbe kwa njia ya maandishi picha video na sauti kama ilivyo program ya Whatsapp.

Mnamo Januari 2021,Telegram ilipita watumiaji milioni 500 wanaotumia kila mwezi. Ilikuwa programu iliyopakuliwa zaidi mnamo Januari 2021 ikipakuliwa mara bilioni 1 duniani kote kufikia mwishoni mwa Agosti 2021. Mnamo Juni 2022, Telegram ilipita watumiaji milioni 700 wanaotumia kila mwezi.

Hivi majuzi Telegram ilizindua usajili wake wa kulipia (Premium) ambao hugharimu Sh.11,500 kwa mwezi, ambao huwapa watumiaji waliojisajili uwezo wa kufikia vipakiaji vikubwa zaidi, upakuaji wa haraka, kipengele cha kutuma sauti kwa maandishi, miitikio ya kipekee ya emoji, na zaidi.