Test2

Simba Yapitisha Majina ya Wagombea Uongozi

Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Boniface Lyamwike, imeweka wazi majina ya waliopita kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambapo wagombea wawili wameondolewa kati ya 21 waliochukua fomu. Taarifa ya kamati hiyo imewataja waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti ni wale wale wawili waliochukua fomu ambao ni Swedy Mkwabi na Mtemi Ramadhani. Katika nafasi ya ...

Read More »

LISHE DUNI NA ULAJI USIOFAA NI ADUI WA MAENDELEO NCHINI-MAJALIWAPicha

    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI    LISHE DUNI NA ULAJI USIOFAA NI ADUI WA MAENDELEO NCHINI-MAJALIWA *Asema ni chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza kama saratani, kisukari na moyo  *Asisiza wananchi kuzingatia ulaji unafaa na kubadili mitindo ya maisha     MAGONJWA yasiyoambukiza yanachangia  kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kasi ya maendeleo yetu kwani gharama za matibabu yake ni kubwa mno, ...

Read More »

WAZIRI MKUU AKATISHA ZIARA DODOMA, AENDA UKEREWE

WAZIR MKUU Kassim Majaliwa amekatisha ziara ya mkoa wa Dodoma na kuelekea Ukerewe Mwanza kuwafariji wananchi waliopatwa na maafa kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere. Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma, ametangaza uamuzi huo leo mchana (Ijumaa, Septemba 21, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chandama, wilayani ...

Read More »

Yanga Yaendele kujiweka Fiti kwa Ajili Yeyote atakeyekuja Mbele

Na George Mganga Klabu ya Yanga imeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United utakaopigwa Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii. Yanga imezidi kujifua chini ya Kocha wake Mkuu, Mkongomani Mwinyi Zahera ambaye amekuwa mbogo kwa wachezaji wasio na nidhamu baada ya kuanza kuwaondoa kambini kila wanapochelewa kuripoti. Kwa mujibu wa Mwenyekiti ...

Read More »

Haji Manara Waangukia Mashabiki wa Simba

Baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa CCM Kirumba, jijini Mwanza, uongozi wa klabu ya Simba umewaomba radhi mashabiki wake. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameibuka na kuomba radhi wa wapenzi, mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa namna walivyoyapokea matokeo hayo ya kusitikisha kwao yaliyosababisha kupoteza alama ...

Read More »

Updete Ajali ya Mv Nyerere Mwanza

RC wa Mwanza, John Mongela amesema idadi ya watu waliofariki kwa ajli ya #MvNyerere kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 94 leo asubuhi. DC Ukerewe amesema Kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 100 na tani 25 za mizigo, lakini kibeba abiria zaidi ya 400.   Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara ...

Read More »

SIMBA YAWEKA REKODI NYINGINE

Klabu ya Simba imeendelea kuweka rekodi kwa msimu wa pili mfululizo kuwa ni timu ya kwanza kwa kutoa mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu Bara. Msimu huu mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda Meddie Kagere ndiye alikuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti msimu huu baada ya kucheza michezo mwili. Msimu wa uliopita Simba ndiyo ilifungulia kwa kutoa mchezaji bora ...

Read More »

Miili 44 ya waliofariki katika Kivuko inavyotolewa majini

Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere kilichozama limesitishwa kutokana na giza na litaendelea leo alfajiri ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema mpaka sasa watu waliyookolewa wakiwa hai ni 37 na waliopoteza maisha ni 44. RC Mongela amesema Kivuko hicho haikujulikana kilikuwa na idadi ya watu wangapi.    

Read More »

Mjue Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka

  DAR E SALAAM NA MWANDISHI WETU, Akiwa ziarani katika Mkoa wa Simiyu, Rais John Magufuli, alimsifu Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka, na kumtaja kama kiongozi mahiri aliyefanya mambo mengi, mazuri kwa muda mfupi. Akasema awali alipopendekeza jina la Mtaka, aliambiwa (vetting) kuwa kiongozi huyo kijana hafai hata kuwa Mkuu wa Wilaya (DC), lakini kazi alizofanya zimemfanya awe RC ...

Read More »

Ndugu Rais Katibu Mkuu CCM awe tumaini letu

Ndugu Rais, ni lini mwokozi wangu atapita kwangu nami nipate kuligusa pindo la vazi lake ili haya ninayowalilia waja wake yafike mwisho? Maskini aliye na raha ya Mungu ana raha ya milele! Chama Cha Mapinduzi kimepata Katibu Mkuu mpya. Na awe tumaini la wenye mioyo iliyopondekapondeka! Katibu Mkuu weka akilini kuwa, umeteuliwa kushika nafasi hiyo kutokana na vile ulivyo sasa. ...

Read More »

MAFANIKIO YOYOTE YANA SABABU (38)

Na Pd. Dk. Faustin Kamugisha Mtandao chanya wa watu ni sababu ya mafanikio. Huwezi kupiga makofi kwa mkono mmoja. “Ukitaka kwenda kwa haraka sana, nenda peke yako. Ukitaka kwenda mbali, nenda pamoja na wengine.” (Methali ya Kiafrika). Hawa wanaotajwa kama ni wengine ni wale ambao wana mtazamo chanya. Ni wale ambao wanapiga makasia mtumbwi wako wa mafanikio ufike ufukweni. Ni ...

Read More »

Ujenzi wa barabara waathiri makazi Temeke

NA ALEX KAZENGA DAR ES SALAAM Wananchi wa Kata ya Makangarawe, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wameulalamikia ujenzi wa barabara za mitaa unaofanywa kwa kiwango cha lami katika mitaa hiyo wakidai kuharibu makazi yao. Ujenzi huo umeanza kutekelezwa hivi karibuni chini ya Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), mradi huo unafanyika pasipo kuwahamisha wananchi ...

Read More »

Polisi yanasa bunduki 180, uhalifu wapungua

  KHALIF MWENYEHERI NA CATHERINE LUCAS, TUDARCO Jeshi la Polisi nchini limekamata silaha 187 katika kipindi cha Juni mwaka jana hadi Septemba mwaka huu, huku vitendo vya mauaji vikipungua kutoka 1,538 na kufikia 1,311 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Jeshi la Polisi, silaha hizo zilizokamatwa katika maeneo mbalimbali nchini zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na kutumika katika ...

Read More »

Maajabu ya viboko kisiwani Mafia

DAR ES SALAAM NA JUMA SALUM Kijiografia, Mafia ni kisiwa kilichoko Bahari ya Hindi, kilometa 120 kusini – mashariki mwa Jiji la Dar es Salaam na kilometa 20 mwambao wa pwani ya Wilaya ya Rufiji. Katika hali ya kushangaza, eneo la katikati la kisiwa hiki kidogo chenye ukubwa unaokadiriwa kuwa karibu nusu ya Kisiwa cha Unguja, wanapatikana wanyamapori aina ya ...

Read More »

Mkurugenzi UCC ahusishwa kashfa nzito

Na Alex Kazenga Dar es Salaam Wafanyakazi zaidi ya 30 wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta (UCC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamo hatarini kupoteza kazi baada ya kituo hicho na matawi yake yote nchini kutakiwa kufungwa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mbinu zinazoratibiwa na menejimenti kukiua kituo hicho. Anayetuhumiwa kufanya mbinu hizo ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo ...

Read More »

Korosho bado ni ‘umiza kichwa’! (1)

Nilifurahi mno Jumatano ya Septemba 5, mwaka huu nipoona katika runinga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gilasius Byakanwa, akiwa katika Kiwanda cha Korosho Tandahimba akitoa uamuzi wa serikali (kwa barua rasmi) kwa mwekezaji wa kiwanda kile kununua korosho kwa kufuata maelekezo ya serikali kupitia mnada wa stakabadhi ghalani. Na kwamba amalizapo kubangua afuate sheria za ununuzi wa korosho kama ilivyoelekezwa ...

Read More »

Jela si mchezo

DAR ES SALAAM NA WAANDISHI WETU Kishindo kikubwa kinatarajiwa kuanza kusikika wiki hii baada ya mabadiliko ya uongozi katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Mtikisiko huo, pamoja na mambo mengine, utawahusisha baadhi ya vigogo wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi. Tayari kuna orodha ndefu ya majina ya watu wanaokusudiwa kufikishwa kwenye ‘Mahakama ya Mafisadi’ kujibu tuhuma zinazowakabili. Kwenye orodha ...

Read More »

Mbunge wa Uganda Robert Kyagulanyi Kurejea Uganda Leo

Mbunge wa Kyandodo Mashariki mwa Uganda, Robert Kyagulanyi ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini humo ajulikanaye kama Bobi Wine anatarajia kurudi nchini Uganda leo akitokea nchini Marekani ambapo alienda kupata matibabu baada ya kupigwa na vyombo vya dola. “Nitarejea nyumbani siku ya jumatatu,licha ya kuwa bado nna hofu lakini Uganda ndio nyumbani ambapo familia yangu na watu wangu wapo.Nina wasiwasi ...

Read More »

KOCHA CHELSEA AWATAJA WAFUNGA MABAO BORA LIGI KUU ENGLAND

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard anaweza kufunga mabao 40 msimu huu na kujishindia tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia, kwa mujibu wa meneja wa klabu hiyo Maurizio Sarri. Kwa mujibu wa BBC, Hazard alifunga mabao matatu dhidi ya Cardiff Jumamosi na kuwawezesha The Blues kupata ushindi wa 4-1. Kufikia sasa amefunga mabao matano katika mechi tano zilizochezwa, moja ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons