Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) na Benki ya KCB wamesaini mkataba wa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2018/19 wenye thamani ya shilingi Milioni 420.

TFF wamefikia makubaliano hayo KCB baada ya wadau mbalimbali kuanza kuhoji juu ya udhami wa ligi hiyo kutokana na kampuni ya Vodacom ambao ndiyo wadhamini wakuu mkataba wake kumalizika.

Licha ya kusaini na KCB, awali ilikuwa inaelezwa kuwa TFF itafanya mazungumzo mengine na Vodacom ya kuweza kuongeza mkataba mwingine lakini haijajulikana mpaka sasa kuwa mazungumzo hayo yamefikia wapi.

Baada ya kuingia mkataba na benki hiyo, Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 inatarajia kuanza Agosti 22 ambapo tayari ratiba ya msimu mzima imeshatoka.

908 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!