Wachezzaji wa Tottenhum Spurs Wakishangilia bao  Tottenhum Spurs imefanikiwa kuwafunga maasimu wao kutoka mji mmoja wa London, Arsenal kwa bao mojo kwa bira, bao pekee la Spurs lilifungwa na Harry Kane kwa kichwa ambapo alinganisha krosi ya Ben Davies

Mchezo huo ulikuwa wa vuta ni kuvute, kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilishindwa kufungana, katika dakika ya 49 mshambuliaji wa spurs Harry Kane aliwainua mashibiki wake vitini baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Ben Davies na kuiandika Spurs bao la kuongoza  na likadumu mpaka filimbi ya mwisho ya mchezo.

Kwa matokeo hayo spurs imepaa mpaka nafasi ya tau ikiziteremsha Chelsea na Liverpool na sasa ipo kwenye nafasi ya tatu ikiwa na point 52 nyuma ya Mashetani wekundu Manchester united ambao wao wanacheza kesho na Newcastle United.

Arsenal wamesalia kwenye nafasi yao ya sita na points zao 45. Matokeo ya leo yamewanufaisha Zaidi Spurs kwani wamepanda nafasi mbili juu, ukilinganisha na Arsenal ata wangeshinda wao wangebaki kwenye nafasi yao ya sita.

Matokeo za mechi nyingine

Everton 3 – 1 Crystal Palace

Stoke City 1 – 1 Brighton & Hove Albion

Swansea City 1 – 0 Burnley

West Ham United 2 – 0 Watford

Manchester City 5 – 1 Leicester City

Ratiba za mechi za kesho ni

Southampton VS Liverpool (15:00)

Newcastle United VS Manchester United (19:30)

Huddersfield Town VS AFC Bournemouth (17:15)

 

 

 

996 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!