Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wamewasili Singapore kwa ajili ya mkutano wao unaoelezwa kuwa wa kihistoria.

Trump aliwasili saa chache tu baada ya Kim kuwasili na ujumbe wake.

Mkutano wao ambao ni wa kwanza utafanyika siku ya Jumanne katika kisiwa cha Sentosa.

Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua wawili hao kukutana.

Mwaka wa kwanza wa Trump katika kiti cha urais ulianza kwa mvutano mkubwa na kurushiana maneno huku Kim naye akiendeleza majaribio ya silaha za nuklia na kukiuka ilani ya kimataifa.

Rais wa Marekani aliapa kupambana ikiwa Pyongyang itaendelea kuitishia Marekani, wote wakipeana majina ya kukebehi.

Korea Kaskazini iliendelea kukaidi na kufanya jaribio la nuklia la sita mwezi Septemba mwaka 2017.

Baadae Kim alitangaza kuwa nchi yake imefanikiwa mpango wake wa kua taifa la nuklia, likiwa na silaha zinazoweza kuifikia Marekani.

Lakini mwanzoni mwa mwaka 2018, Korea Kaskazini ilianza kuboresha mahusiano na Korea Kusini kwa kupeleka timu na ujumbe kwenye michuano ya Olimpiki mjini Pyeongchang.

Mwezi Machi, Donald Trump aliushangaza ulimwengu kwa kukubali mwaliko kutoka kwa Kim wa kukutana ana kwa ana.

By Jamhuri