MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), leo Ijumaa Januari 5, 2017 kwa mara ya kwanza tangu ajeruhiwe amezungumza na waaandishi wa habari jijini Nairobi nchini Kenya anakopatiwa na kusema kilichotokea kwake kwa maoni yake ilikuwa ni mauaji ya kisiasa moja kwa moja ‚ÄúPolitical Assassination‚ÄĚ.

Lissu ameeleza kuwa risasi 16 zilimpiga mwilini mwake huku risasi nane zikitolewa Dodoma na risasi saba kutolewa jijini Nairobi ambapo amebakiwa na risasi moja mwilini mwake.

Amefafanua kuwa sehemu alipopigiwa risasi ni nyumbani kwake alipopangiwa na Bunge kwa kuwa yeye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni hivyo eneo ambalo anakaa ni sehemu palipo salama lakini alimiminiwa risasi 16 na waliofanya hivyo hawajulikani walipo huku akisema watu waliohesabu risasi zilizopiga gari yale ziko 38 lakini 16 ndizo zilizompata mwilini.

Mbunge huyo ambaye amemaliza miezi minne hospitalini hapo akitibiwa tangu Septemba 7, 2017 amesema alipelekwa akiwa vipande vipande lakini madaktari pamoja na wataalamu wa hospitali hiyo wameweza kumfanya awe alivyo hivi sasa.

Aidha Lissu amewataja madaktari wawili ambao ni Vincent Mutiso ambaye ni daktari bingwa wa mifupa na daktari Fred Mongea ambaye alihakikisha anapata fahamu na kurudi sawa na kuongeza tukio lililomfikisha Nairobi lilishtua sana hivyo anawashukuru wote waliomchangia fedha, damu na kumuombea ili aweze kupona na kufikia alivyo hivi sasa.

Lissu anatarajiwa kusafirishwa kwesho Januari 6, kwenda barani Ulaya kwa ajiri ya matibau zaidi.

 

2602 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!