Kwenye ukurasa wake wa Instagram Mbunge wa Singida Kaskazi, Tundu Lissu amemtolea povu Lemutuz.

Tundu lissu alisema haya “Leo (Jana) nimeonyeshwa post iliyopo kwenye Instagram account ya William Malecela aka Lemutuz.

Kwenye post yake, Lemutuz amedai kwamba mimi ni rafiki yake mkubwa na wa miaka mingi, kabla vijana wengi wanaopiga makelele mitandaoni hawajazaliwa.

Lemutuz ameeleza kwamba mwaka 2010 alinipokea Uwanja wa Ndege wa John F. Kennedy, mjini New York, nilipoenda kwenye mahafali ya dada yangu. .

Amewaambia wasomaji wake kwamba alinichukua kwenye gari yake binafsi kutoka JFK hadi Connecticut kwenye graduation ya dada yangu aliyodai ilikuwa Connecticut State University. .

Ili kuthibitisha kauli zake, Lemutuz ameambatanisha picha niliyopiga naye, ambayo nitaielezea shortly.  “  Alisema Tundu Lissu kwenye Ukurasa wake Instagram

Aliendelea kusema:

“Naomba kuweka ukweli wa kauli za Lemutuz wazi ili kuweka rekodi sawa.

Kwanza, nimemfahamu Lemutuz tangu mwezi Mei, 2011. Nilikutana naye mara ya kwanza kwenye mahafali ya mdogo wangu kaka (sio dada) Vincent Mughwai, aliyekuwa anasoma Bridgeport University (sio Connecticut State University). Kama nakumbuka vizuri, Lemutuz alikuwa MC kwenye shughuli hiyo. Na siku hiyo kulikuwa na Watanzania wengine wengi waishio Marekani. .

Lemutuz hakunipokea mimi JFK wala kunipeleka Bridgeport, Connecticut, kwenye gari yake binafsi. Hatukuwa tunafahamiana kabla ya kukutana kwenye graduation ya kaka Vince, siku kadhaa baada ya mimi, mke wangu na ndugu zangu wengine kuwasili Marekani. .

Pili, ni kweli tulipiga picha ambayo ameitoa kama uthibitisho wa ‘urafiki’ wetu. Siku hiyo, kama ilivyo kwenye shughuli kama hizo, nilipiga picha na Watanzania karibu wote waliohudhuria graduation hiyo.

Kama Lemutuz, wengi wa niliyopiga nao picha nilikuwa siwafahamu kabisa kabla ya kukutana nao siku hiyo. .

Tatu, tangu siku hiyo sijawahi kufanya mawasiliano na Lemutuz ya aina yoyote. Nakumbuka tu kukutana na kusalimiana nae bungeni mwaka 2012, wakati alipokuja Dodoma akitaka kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. .

Mimi sijajua sababu ya Lemutuz kutaka kulazimisha urafiki na mimi usiokuwepo. Yeye ni rafiki mkubwa wa Bashite na mpiga debe wa Rais Magufuli. .

Mimi ni mpinzani mkubwa wa Magufuli na nimelipa gharama kubwa kwa sababu ya msimamo wangu tangu Magufuli aingie madarakani. .

Huo ‘urafiki mkubwa’ unaodaiwa kuweka kati yangu na Lemutuz msingi wake ni nini???
.

Mwisho, ukitaka kuongopa hadharani basi angalau uwe na kumbu kumbu sahihi. Lemutuz anadai tulikutana 2010 wakati ilikuwa Mei 2011. .

Anadai nilikwenda kwenye graduation ya dada yangu (ambaye hata jina hakumtaja!) wakati ilikuwa graduation ya kaka yangu Vincent Mughwai. .

Anadanganya ilikuwa Connecticut State University wakati ilikuwa Bridgeport University. Anadai alinipokea JFK wakati nilipokelewa na kaka yangu Vincent. .

Na tangu nimepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na wanaoitwa ‘watu wasiojulikana’, rafiki yangu mkubwa huyu hajawahi kunitumia hata kadi ya pole!!! .

Huu ni urafiki feki wa kuwadanganyia Watanzania wasioelewa. .

Msidanganyike!!!

 

Update ya Hali ya Tundu Lissu, Anaendelea powa na anaendelea kufanya mazoezi ya viungo

1642 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!