Tuzo za Mo Awards Kutolewa leo

Tuzo za Simba Mo Awards zinafanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zitakuwa maalum kwa watu wa klabu hiyo waliofanikisha Simba kufanya vizuri kwa msimu wa 2017/18.

 

Wanachama, viongozi, mashabiki na matawi ya klabu hiyo yatahusishwa katika ugawajwi wa tuzo hizo zitazofanyika leo kuanzia saa 12 kamili jioni.

 

Kwa mujibu wa mwanzilishi ambaye ni mwekezaji mpya wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’, amesema lengo mahususi la kuanzisha tuzo hizo ni kutambua mchango wa waliofanikisha Simba kufikia hapo ilipo.

 

Baadhi ya vipengele ambavyo vitakuwepo katika ugawajwi wa tuzo hizo ni mchezaji bora wa mwaka, kiungo, mshambuliaji, shabiki na zinginezo.

 

706 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons