Mwenyekiti wa tume ya muungano wa bara Afrika Moussa Faki Mahamat

Umoja wa Afrika unasema matamshi ya yanayodaiwa kutolewa na rais wa Marekani Donald Trump kuhusu bara la Afrika ni wazi kwamba ni ya ubaguzi wa rangi.
Msemaji wa umoja huo , Ebba Kalondo, amesema toni la matamshi hayo lilikera hata zaidi ikikadiriwa idadi ya Waafrika waliouzwa kama watumwa Marekani.
Umoja huo unataka rais Trump aombe radhi.
Inadaiwa kwamba rais Trump alitoa matamshi hayo dhidi ya Africa, Haiti na Elsavador kwenye ikulu ya White house katika mkutano na wabunge wa congress.

Rais Trump alitoa matamshi hayo katika afisi yake katika Ikulu ya Whitehouse
Baadaye rais Trump alikana kutoa matamshi hayo.
Siku ya IJumaa bwana Trump alituma ijumbe wa Twitter akisema kwamba lugha aliyotumia wakati wa mkutano wake na wabunge wa Congress ili kuzungumzia swala la uhamiaji ilikuwa ngumu.
”Matamshi yalitolewa na Trump hayana heshima ya tofauti iliopo na haki za kibinaadamu”.
Uliongezea: Huku tukionyesha kushangazwa kwetu , Umoja wa Afrika unaamini pakubwa kwamba utawala mpya wa Marekani haulielewi bara la Afrika na watu wake.
”Kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya utawala wa Marekani na mataifa ya Afrika”.

By Jamhuri