Imeelezwa uongozi wa Gor Mahia FC umeshangazwa na kitendo cha mshambuliaji wao tegemeo, Meddie Kagere kujiunga na klabu ya Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Wakati Kagere akiwa nchini Kenya ikiwa ni wiki kadhaa zimepita baada ya mashindano ya SportPesa Super Cup kumalizika, aliomba ruhusa kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya masuala yake binafsi.
Lakini kilichokuja kuwashangaza ni Kagere kuchukua ndege ya kuelekea jijini Dar es Salaam akiwa na wakala wake kwa ajili ya kuja kufanya mazungumzo na Simba kisha kusaini mkataba wa miaka miwili.
Kitendo hicho kimewaumiza Gor Mahia na kuona kama Kagere ni msaliti wakati walikuwa kwenye mazungumzo naye ya kuongeza mkataba mwingine baada ya ule aliokuwa anao ndani ya klabu hiyo kumalizika.
Aidha, imeelezwa viongozi wa Gor Mahia wameshangazwa na Kagere kushindwa kuwaeleza hali halisi kuwa alikuwa anataka kusafiri kuelekea Tanzania na badala yake alidanganya kuwa anaenda kwao Rwanda.
Tayari Kagere ni mali ya Simba na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho katika michuano ya KAGAME inayotaraji kuanza Jun

By Jamhuri