Upinzani Njia Panda

Vyama vya upinzani nchini vinakabiliwa na hali ngumu ya kustawi katika kile kinachoonekana kubuniwa na kutekelezwa kwa mkakati unaolenga kuviangamiza. Wasomi na wanasiasa wanaiona

hatari hiyo, na wanasema juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa kuhakikisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiendelei kuvimaliza vyama vingine vya siasa.

Kwa siku za karibuni, kundi kubwa la wafuasi wa upinzani limejiunga na linaendelea kujiunga CCM kwa kile kinachotajwa kuwa ni kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Tayari Rais Magufuli, amewateua viongozi kadhaa wa upinzani na kuwaingiza kwenye Serikali. Wanaojulikana kwa wengi ni Anna Mgwira (ACT Wazalendo) ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Profesa Kitila Mkumbo (ACT Wazalendo) ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji; na Dk. Wilbroad Slaa (aliyejiuzulu Chadema) ambaye wiki iliyopita ameteuliwa kuwa Balozi. Mtikisiko mkuu ulivikumba vyama vya upinzani wiki iliyopita kwa wanachama wake kujiungaCCM.

Miongoni mwao ni Profesa Mkumbo, Samson Mwigamba na Edna Sunga (wote ACT-Wazalendo), Lawrence Masha, Patrobas Kitambi, David Kafulila (wote CHADEMA); na aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi, na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye. Medeye ametangaza kukihama chama cha United Democratic

(UDP) kinachoongozwa na John Cheyo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. George Kahangwa, ameliambia JAMHURI kuwa huu ni wakati kwa vyama vya siasa vya upinzani kujitathimini upya kupata jawabu la hatima yao.

Anasema siasa ni mchezo wa aina fulani unaohitaji ubunifu wa kila mara kwa chama husika ili kuendelea kujijengea uhalali wa kukubalika kwa wapigakura,vinginevyo vinaweza kupotea. “Wanapaswa kuwa makini na haya matukio ya kuondokewa na wanachama na viongozi wao wanaoendelea kuhama kila siku na kujiunga na chama tawala vinginevyo huenda mwaka 2020 wakajikuta pabaya,” anasema Dk. Kahangwa. Ametetea uhuru wa mtu kujiunga na chama anachotaka, lakini anaonya kuwa kuna madhara makubwa hasa kwa vyama vidogo.

 Bofya Hapa Kusoma na kurasa za ndani

TUPIA MAONI YAKO
478 Total Views 6 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!
Show Buttons
Hide Buttons