Katibu wa Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM)  mkoa wa Dar es Salaam amewataka vijana wa Jumuiya ya vijana mkoa wa Dar esSalaam kusimamia Misingi ya Jumuiya hiyo kwani ndiyo nguzo kuu ya chama inayozalisha viongozi mbalimbali wa Chama na serikali.
Kauli hiyo ameitoa jana Jumamos Katika ukumbi wa Anatogro jijini Dar es Salaam alipokuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda Wakati wa uzinduzi Wa Baraza la Vijana wa UVCCM la utekelezaji.
Akielezea Misingi ya chama hicho amesema UVCCM ni nguzo kuu inayopaswa kuzingatiwa Katika mstakabali wa Taifa
 Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala amesema kuwa Baraza lake lilifanya ziara ya kutembelea kila wilaya za mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kukagua fedha zinazotolewa na serikali kwa kila halmashauri za vijana kwa ajili ya mikopo ili kuweza kujishughulisha Katika kuleta maendeleo.
1487 Total Views 12 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!