Meli tatu zimeegesha nchini Hispania,zikiwa mamia ya wahamiaji waliokolewa majini wiki iliyopita wakitokea nchini Libya.Wameorodheshwa na kuendelea kupatiwa matibabu na misaada.

Serikali ya Hispania imekubali kuwachukua,baada ya Italia na Malta kukataa meli hizo zilizowaokoa wahamiaji hao kuegesha katika bandari.Tukio hili limezua mjadala wa kisiasa Ulaya.

Shrika la msalaba mwekundu,limezitaka nchi za jumuiya ya Ulaya,kuiga mfano wa Hispania kuonyesha mshikamano katika suala la wahamiaji.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Valencia,Mratibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka Aloys Vimard, watu waliopo ndani ya meli hizo wamelazimika kusubiria Zaidi ya wiki moja,wakati wanasiasa wakijadiliana hatima yao.

“Jambo ambalo hatuhitaji kulisahahu ni maisha ya watu,ambayo serikali za Ulaya zinayapuuza.Watu hawapaswi kuchukuliwa kama mizigo inayotarajiwa kushushwa mahala.Kila mmoja,yeyote ambaye amekumbwa na hali isiyo ya kawaida baharini ni lazima apewe haki sawa.Hatujui ni nini cha tofauti kibinadamu kilichopo kwa binadamu waliomo ndani ya Aquarius,kwanini wasiruhusiwe kufika kwenye bandari salama kwa wakati.Wakati ni jambo la usalama kwa watu hawa kuletwa sehemu salama,lakini mjadala wa wanaiasa kujadili maisha yao umechukua juma zima hadi sasa.”Aloys Vimard

Naye Naibu mkurugenzi wa kitengo cha dharula cha Jorge Suarez amesema kuwa wahamiaji wengi waliomo ndani ya meli hawana matatizo makubwa kiafya.

Afisa mkuu wa uhamiaji na Polisi wa mpkani Bernardo Alonso amefafanua haki za wahamiaji hao watakazopata wakiwa nchini Hispania.

“Serikali ya Hispania imechunguza na kuona kwamba,wataruhusiwa kuingia kwa sababu zisizo za kawaida za kawaida kwa siku 45.Baada ya uchunguzi wa Polisi kukamilika,watasaidiwa na asasi zisizo za kiserikali zinazofanya kazi chini ya wizara ya kazi.Mamlaka ya Hispania imebaini kuwa wote wanastahili kupewa ulinzi wa kimataifa kama wakimbizi,ambapo uchunguzi utafanyika mtu na mtu.Si jambo litakalochukuliwa jumla jumla tu,lakini ni kwa wale watakaokidhi vigezo ndiyo ambao hatua zaidi za kisheria zitaendelea mbele.”Bernardo Alonso

Raia hao walikuwa wakivuka kuelekea nchi za Ulaya wakitokea Libya.

By Jamhuri