Wananchi Kyela wajitokeza kupiga kura

Wananchi wa kata ya Mwanganyanga katika mji mdogo wa Kyela, jijini Mbeya leo asubuhi Jumapili Agosti 12, 2018 wamejitokeza kupiga kura kuchagua diwani.

Msimamizi wa Uchaguzi katika kata hiyo, Amos Basiri amesema vituo vyote vimefungulia saa 1 asubuhi na wananchi wameanza kufika vituoni saa 12.

“Tunashukuru hadi sasa upigaji kura umeanza na hakuna shida yoyote tuliyoipata wala malalamiko kutoka kwa wagombea au wapiga kura wenyewe. Kila kitu kinakwenda vizuri,” amesema.

Amesema wananchi 2,698 waliojiandisha ndio wanaoshiriki upigaji kura kumchagua diwani, kubainisha kuwa wagombea wapo watano.

Amewataja wagombea hao kuwa ni Danford Mwambije (ACT-Wazalendo), Alex Mwinuka (CCM), Kanyiki Andembwisye (Chadema), Aman Mwaijenga (CUF) na Deus Mwakilasa (NCCR-Mageuzi).

Andemwisye na Mwinuka wameieleza MCL Digital kuwa mawakala wao wote wamefika na wanaendelea kutekeleza majukumu yao, hawajapata taarifa za tatizo lolote hadi sasa.

839 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons