Mashambulizi ya anga Syria
Mashambulizi ya anga Syria

Takriban watu 23 wameuawa hadi sasa katika mashambulio ya anga ya vikosi vya serikali nchini  Syria katika eneo la mashariki mwa Ghota karibu na mji wa Damascus, kuna kodaiwa kuwa ni ngome ya waasi.

Waangalizi wa haki za binadamu kutoka Uingereza waliopo katika maeneo hayo wameelezea hali hiyo na madhara kwa watu kutokana na mashambulio hayo.

Umoja wa mataifa umetoa wito kusitishwa kwa mapigano hayo mapema iwezekanavyo. Awali majeshi ya Syria yalidai kuwa vikosi vya anga vya Israel vilishambulia ngome za kijeshi zilizopo karibu na mji mkuu Damascus.

Raia mmoja wa kutoka eneo la Douma nje kidogo ya Damascus ambaye hakutaka kutajwa jina lake alieeleza juu ya hali ilivyo kufuatia mashambulizi hayo

“Tuna watu 19 waliojeruhiwa. Nyumba zimeharibiwa vibaya kutokana na mashambulizi haya ya anga,ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya kumi hapa wakiwemo akina mama na watoto. Hapa Douma pekee yake tangu kuanza kwa mashambulizi haya watu 33 waliouawa, ukiongeza na wengine 19 waliouawa al-Ghouta.

Tuna maji na chakula lakini tatizo ni huduma za dawa. Tuna Zaidi ya majeruhi 700 hapa wanaohitaji huduma ya haraka ya afya,wanaweza kufa muda wowote.”.

Vikosi vya uokoaji mashambulizi hayo ya anga yamelenga maeneo kadhaa katika miji ya mashariki mwa Ghuta kuanzia hapo jana, hali inayosababisha makazi ya watu kubomoka.

Zaidi ya watu 130 hadi sasa wanahofiwa kufa tangu vikosi vya serikali ya Syria vilipoanzisha mashambulizi ya anga siku ya jumatatu wiki hii. Zaidi ya watu 400,000 wapo katika eneo la mapigano Mashariki mwa mji wa Gouta tangu mwaka 2013.

 

885 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!