Ilala kuanza ujenzi wa barabara ya Buguruni kwa mnyamani ndani ya wiki moja kuanzia leo ili kuondoa kero kwa wananchi wa eneo hilo. 

Waziri Jaffo ametoa agizo hilo baada ya kufanya ukaguzi katika barabara hiyo inayoelekea katika hospitali ya Buguruni kwa Mnyamani na kuutaka uongozi wa wilaya ya Ilala kusimamia ujenzi huo mara moja.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la segerea Bhona Kaluwa amemshukuru waziri Jaffo kwa kukagua na kufanya maamuzi ya ukarabati wa barabara hiyo inayohudumia pia wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali ya Buguruni kwa Mnayamani.

Barabara hiyo ya Buguruni kwa Mnayamani imekuwa kero kubwa kwa watumiaji wake kutokana na kuwa na mshimo makubwa yanayosababisha kukwama kwa shughuli nyingi za kibinadamu.

1112 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!