Mmoja wa viongozi wa Yanga nchini Ethiopia, Hamad Islam, amesema kwamba; “Wachezaji wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku na tuko tayari kwa mchezo. Hali ya hewa ni nzuri siyo baridi kali sana, inafanana na ya Dar ilivyo kwa sasa, mechi ni saa 10 jioni.”

 

“Tuombeane kwani Yanga imebeba bendera ya nchi kwa sasa, tunataka tuhakikishe tunapata bao, hatujaja hapa kujilinda,” alisema kiongozi huyo.

 

Kiungo mahiri wa Yanga, Papy Tshishimbi amenukuliwa na Gazeti moja la Ethiopia akisema; “Ni mechi ngumu lakini tuna timu nzuri, Tupo kwenye hali  nzuri, tutalinda ushindi wetu na kuongeza zaidi.

 

“Changamoto tuliyonayo ni kwenye ushambuliaji. Tukifuzu kwenye hatua ya makundi tunahitaji kujiweka sawa zaidi kwa kuongeza nguvu.”

 

1212 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!