Kikosi cha Yanga kipo mjini Morogoro kikiendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Yanga itashuka dimbani Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 19 2018 kumenyana na Alger kutoka Alger wakiwa na kumbukumbu mbaya katika mechi ya mkondo wa kwanza.
Yanga iliruhusu mabao manne kwa sufuri huko Algiers, Algeria na mpaka sasa ikiwa ina alama moja pekee katika kundi ambalo timu zingine zilizopo ni Rayon Sports ya Rwanda na Gor Mahia FC ya Kenya.
Kuelekea mechi hiyo, Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera, anaamini Yanga wanaweza wakafanya vizuri dhidi ya wapinzani wao.
Zahera ana imani hiyo kulingana na mazoezi anayowapa vijana wake akizingatia kufanyia marekebisho juu ya mapungufu kadhaa ambayo yamejitokeza katika mechi zilizopita za mashindano hayo.

By Jamhuri