Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City kikiwa mjini Mbeya leo.

Tayari kikosi hicho kimeshaondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mbeya kwa usafiri wa ndege ambapo kesho kitakuwa na kibarua hicho.

Yanga inacheza na Mbeya ikiwa ina siku moja tangu irejee nchini ikitokea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaita Dicha.

Mabingwa hao watetezi wa ligi wako nyuma kwa michezo miwili dhidi ya Simba ambao wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 11 na Yanga.

1157 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!