Yanga Yakubaliwa Kujiondoa Kagame Cup

Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limekubali maombi ya Yanga kujiondoa katika mashindano ya KAGAME baada ya kutuma barua iliyoeleza kuomba kujitoa

Yanga ilituma barua kupitia TFF ikiomba kujiondoa ili kuwapa nafasi wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya.

Barua hiyo ilieleza kuwa ratiba ya michuano imekuwa si rafiki kwao na itakuwa inawabana sababu wanapaswa kuwajibika kwenye mashindano ya shirikisho pia wachezaji wake wengi hawana mikataba.

Kutokana na maombi hayo, CECAFA wamemua kuuwaalika Vipers SC ya Uganda kuchukua nafasi ya Yanga ambapo katika kundi C wataungana na Simba, Dakadaha ya Somalia na St. George ya Ethiopia.

Michuano hiyo inatarajia kuanza kurindima June 28 mwaka huu na kumalizika Julai 13 2018.