Sheria inatumika kuiua reli hiyo, wafanyakazi hoi
Mizigo tani 20,000 yarundikwa kwa mwaka mzima
Siku chache baada ya Serikali ya China kutangaza nia ya kuisadia Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) vifaa vitakavyoifufua reli hiyo, Chama cha Wafanyakazi TRAWU-TCPC kimesema njia pekee ya kuanza kuifufua reli hiyo ni kuondoa uongozi wa mameneja wote wa vitengo, na kuweka mameneja wapya wenye uwezo wa kufanya kazi kibiashara zaidi.

“Hivi tumegundua kosa letu sasa. Miaka ya nyuma ilikuwa tunapambana kuondoa madarakani Mkurugenzi Mkuu, lakini sasa tumebaini kumuondoa Mkurugenzi Mkuu pekee si suluhisho. Tatizo ni hawa mameneja wa vitengo.

“Unakuta meneja wa procurement (manunuzi) anaagiza mafuta ya wiki mbili, mafuta hayo yakitumika yakaisha ndipo anaanza taratibu za kuagiza mafuta mengine. Matokeo yake treni zinazimikia njiani.

“Mizigo ya wateja inarundikana hapa Tazara, halafu tunalalamika kuwa kampuni haina hela. Hela itapatikana wapi wakati uongozi hautoi vitendea kazi muhimu

“Mimi nasema ikiwa msaada wa China unakuja chini ya mameneja wa aina hii tulionao, wanaoshindwa kununua hata mafuta, ni heri msaada huo usije kabisa. Itakuwa sawa na kumwaga ndoo ya maji baharini,” Mwenyekiti wa Tawi la TRAWU-TCPC, Yassin Mleke, ameiambia JAMHURI mwishoni mwa wiki.

By Jamhuri