Na Daniel Limbe, JamhuriMedia,Chato

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Dickson Jackobo,mkazi wa Kasenda Muganza,wilayani Chato mkoani Geita anadaiwa kumuua kwa panga mke wake, Kasaka January (40), kwa kile kinachoelezwa kuwa ni uchu wa mali.

Mauaji hayo yametekelezwa usiku wa kuamkia leo, ikiwa ni siku chache tangu wananchi wa kata ya Muganza kuteketeza kwa moto kituo chao cha Polisi, hali iliyosababisha kukosekana kwa huduma za kipolisi katika eneo hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Kamishina Msaidizi wa Polisi, Saphia Jongo,amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo ametoroka na jitihada za kumtafuta zinaendelea ili aweze kutiwa mbaroni.

“Mauji hayo yametokana na tamaa ya mali…huyo mama alikuwa na mali na alikuwa na watoto ambao hakuzaa na huyo mumewe…kwa hiyo kitendo cha kuwahudumia watoto wake hakikumfurahisha huyo mumewe…lakini pia huyo mume amekuwa na tuhuma za kumuibia mali mkewe.

“Huyo baba alikuwa anamilikiwa na huyo mkewe na inaelezwa kuwa hivi karibuni alimwibia betri 40 za N 70…baada ya mke kugundua amesema mwizi wangu nimeshamjua na nitamchukulia hatua…kwa hiyo kauli hiyo ukichanganya na mengine tunaamini ndiyo chanzo cha mauaji hayo”amesema Jongo.

Hata hivyo amedai kuwa mauaji hayo yalifanyika muda mfupi baada ya watoto wa marehemu kuondoka kwenye nyumba ya wazazi wao walimo kuwa wakitazama televisheni ambapo walielekea kwenye vyumba nyingine wanayolala na baada ya muda mfupi walianza kusikia yowe ya mama yao akiomba msaada kutokana na mapanga aliyoakuwa akikatwa.

“Baada ya kelele hizo binti mmoja wa marehemu alisogea karibu kumsaidia mama yake lakini baba alivyofungua mlango alikwenda kumkata panga binti yake lakini alifanikiwa kulikwepa na baba akapata upenyo wa kukimbia” amesema Jongo.

Mkuu wa Wilaya ya Chato,Deusdedith Katwale, amethibitisha kutokea mauaji hayo na kuwataka wana ndoa kuheshimiana kwa misingi ya viapo vya ndoa zao badala ya kuendekeza migongano ya umiliki wa mali.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kutumia muda wao kuielimisha jamii kutambua thamani ya ndoa na kwamba wanaposhindana ni vyema wafuate sheria na taratibu za miongozo ya imani zao.

Mmoja wa ndugu wa karibu wa marehemu, Costantine Matogo,amesema kabla ya mauaji hayo mtuhumiwa alijifungia ndani na mkewe kisha kuanza kumshambulia kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chato,Madili Sakumi,amekiri kupokea mwili wa marehemu Kasaka,na kudai kuwa umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya taratibu zai

By Jamhuri