Na Jumanne Magazi, JakhiriMedia, Dar ex Dalaam

Benki ya Maendeleo ikishirikiana na Kariakoo Wamachinga Asociaton (KAWASSO) leo Mei 7 2024, zimezindua Mradi wa Ujenzi na Nyumba za Makazi kwa Wamachinga wa Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi milioni 500, na kuwanufaisha wafanyabiashara 500.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Maendeleo Benki Ibrahim Mwangalaba Amesema mradi huo utakaojulikana kama Machinga Plot Finance.

Mwangalaba amesema mwaka 2021, benki hiyo ilianzisha utaratibu wa kuwasaidia wafanyabiashara ndogo ndogo, wa Soko la Kariakoo na masoko mengine yaliyopo Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema walengwa wa kuu wa mradi huo uliotiwa saini hii leo ni pamoja wafanyabiashara wadogo ambao wanatambuliwa na kuidhinishwa na Serikali kufanya biashara katika maneno ya masoko maarufu kwa jina na vizimba.

Akifafanua zaidi, Mwangalaba amesema katika kipindi cha miaka 3 na nusu Maendeleo Benki imeweza kutoa kiasi cha billion 9.8 kwa wamachinga wapatao7000 ambapo hadi sasa kiasi cha Billioni 7.5 zimeisharejeshwa na bilioni 2.3 zikiwa bado zipo mikononi mwa wafanyabiashara hao ambao wanaendelea kulipa vizuri.

Awali amesema baada ya kupitia kwa makini maombi ya ya KAWASSO, kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo wamekubaliana kununua viwanja hivyo.

Wakati huo huo,, Mkurugenzi huyo ametaja eneo la mradi huo nakudai kuwa hadi sasa tayari wameshapata zaidi ya hekali 89, katika Kijiji cha Magoza kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Mwangalaba ameendelea kusema ilikufanikisha lengo hilo, Tayari Benki hiyo ikishirikiana na KAWASSO wameingia makubaliano na kampuni ya Urasilimishaji Ardhi ya SEMSIC LAND CONSULTANT LIMITED, ambapo mpango Huwa utawawezesha Wamachinga wa MKOA WA Dar es Salaam kupata viwanja kwa bei ya Shilingi Mil 1 kwa kiwanja kimoja, huku wakitakiwa kuresha kidogo kidogo kwa muda WA miezi 12.

Vilevile Mkurugenzi huyo amesema wao kama Maendeleo Benki wakitambua Jitiahada zinazofanywa na Serikali ili kukuza Uchumi na kupunguza umaskinu Serikali haiwezi kufanikiwa bila kushirikiana na Sekta Binafsi hivyo na wao wameona Bora waunge mkoano jitiahada hizo.

Mwenkiti wa KAWASSO, Namoto Yussuf Namoto

Kwa upande wa Mwenkiti wa KAWASSO, Namoto Yussuf Namoto amesema wao wameishukuru benki hiyo kwa kitendo cha kuunga mkono juhudi zao ambapo Leo historia imeandikwa katika kufanikisha kutiwa Saini kwa mkataba wa Ujenzi na Utekelezwaji wa Mradi huo amesema Namoto.

Maendeleo Benki Ibrahim Mwangalaba Ames

By Jamhuri