
Nini kinaendelea Uwanja wa Ndege Chato?
Na Daniel Limbe, Jamhuri Geita Wakati kukiwa na uvumi kwamba Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita umetelekezwa na sasa unatumika kwa kuanikia nafaka, hali sivyo ilivyo. Uwanja huu bora na wa kisasa uliojengwa wakati wa utawala wa Awamu ya Tano wa Rais Dk. John Magufuli, ulilalamikiwa katika mitandao ya kijamii, ukitajwa kutokuwa na faida…