



Rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu ameapishwa leo kuwa kiongozi wa taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika linalokabiliwa na changamoto nyingi.
Anaingia rasmi madarakani huku raia wakiwa na matumaini mapya ya maisha bora na masuala mengine ambayo serikali yake inatarajiwa kuyaboresha.
Bola Tinubu, gavana wa zamani wa jiji la Lagos ambalo ni kitovu cha uchumi Nigeria amechukua nafasi ya alliyekuwa Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari. Ataiongoza nchi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa taifa la tatu kwa wingi wa watu itakapofika mwaka 2050. Tinubu mwenye miaka 71, ameahidi kuendeleza juhudi za Buhari za kuendeleza demokrasia katika nchi inayokabiliwa na mizozo mingi ya kiusalama, umasikini na njaa masuala ambayo yamekuwa yakiwakasirisha raia.
Tinubu alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa Februari 25 aliposhinda kwa kura milioni 8.8 na idadi ya kura zinazotakiwa kwenye theluthi mbili ya majimbo yote ya Nigeria.
Licha ya kuchaguliwa kwake kuendelea kupingwa mahakamani na vyama vya upinzani na miongoni mwa vijana walio wengi, Licha ya kuchaguliwa kwake kuendelea kupingwa mahakamani na vyama vya upinzani na miongoni mwa vijana walio wengi, Tinubu ameahidi kuwaunganisha Wanigeria. Ilani yake ya “matumaini mapya” inatoa vipaumbele katika kutengeneza nafasi za kazi za kutosha na kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani, uwekezaji kwenye kilimo na miundo mbinu ya umma.
Vipaumbele vingine vinahusisha kutoa nafasi za kiuchumi kwa watu masikini pamoja na kuwa na kuwa na mfumo bora wa usalama wa taifa ili kukabiliana na changamoto zote za kiusalama.
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wanasema ahadi na matumaini yaliyotolewa na Tinubu yanakumbusha kile alichoahidi Buhari alipochaguliwa kuwa rais mwaka 2015. Vipaumbele vyake navyo vilijikita katika kupambana na vitisho vya usalama na kuukuza uchumi lakini aliishia kushindwa kufikia matarajio ya walio wengi.
Kati ya waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Bola Tinubu ni mwakilishi maalumu wa Rais wa China Xi Jing Ping, ikiwa ni kulingana na taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya China
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amezitaka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zishirikiane kutumia rasilimali zilizopo kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Jumuiya hiyo.
Dkt. Tulia ameyasema hayo wakati akitoa neno la shukran kwa niaba ya Maspika wenzake baada ya Rais wa Jamhuri ya Seychelles Mhe. Wavel Ramkalawan kufungua Mkutano wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Kibunge la nchi za SADC (SADC-PF) unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Eden Blue uliopo Mahe nchini Seychelles leo tarehe 27 Mei, 2023.
Akitoa mfano wa ushirikiano huo, Dkt. Tulia amesema “nchi wanachama wa SADC wanaweza kutumia mafanikio yanayopatikana kwenye sekta ya uvuvi nchini Seychelles na vivyo hivyo Tanzania inaweza ikatumika kutatua changamoto za uhaba wa chakula unazozikabili nchi nyingine katika Jumuiya hiyo.”
Aidha, Dkt. Tulia anatarajiwa kuitaarifu Kamati hiyo juu ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa hilo unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai 2-8, 2023 Jijini Arusha, ambapo Bunge la Tanzania ndilo mwenyeji wa Mkutano huo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akichangia mada wakati wa Mkutano wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Kibunge la nchi za SADC (SADC-PF) unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Eden Blue uliopo Mahe nchini Seychelles leo Mei 27, 2023
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimia na kuteta jambo pamoja na Rais wa Jamhuri ya Seychelles Mhe. Wavel Ramkalawan wakati wa Mkutano wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Kibunge la nchi za SADC (SADC-PF) unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Eden Blue uliopo Mahe nchini Seychelles leo Mei 27, 2023
.
Mahakama ya Rufaa nchini Ufaransa, imeshikilia kifungo cha miaka mitatu jela, dhidi ya rais wa zamani Nicolas Sarkozy kwa kosa la ufisadi na kushawishi kupewa taarifa kuhusu uchunguzi dhidi yake.
Katika uamuzi wa mahakama hiyo ya rufa jijini Paris, kiongozi huyo wa zamani wa Ufaransa, anaweza tumikia kifungo chake nyumbani akiwa amevalia kitambulisho cha kuonyesha uamuzi huo.
Sarkozy alipewa kifungo cha miaka mitatu jela kwa makosa ya kujaribu kushawishi jaji kwenye kesi nyingine tofauti.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 68, alikuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kutakiwa kufungwa jela.
Alihukumiwa kwa kujaribu kupata taarifa kuhusu kesi aliyokuwa anakabiliwa nayo mwaka wa 2014 baada yake kuondoka ofisini.
Inadaiwa kuwa baada yake kumaliza hatamu yake, alikata kupata taarifa kuhusu kesi yake na iwapo jaji angefanya hivyo, angepewa kazi yenye kiwango cha juu.
Rais huyo wa zamani pia alizuiwa kuwania katika nyadhifa yoyote ya umma kwa miaka mitatu.Hii ni mojawapo ya kesi anazokabiliwa nazo kiongozi huyo wa zamani wa Ufaransa, tuhuma ambazo hata hivyo amezikana zote.
Nicolas Sarkozy alihudumu kama rais kwa muhula mmoja mwaka wa 2007
Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki imemchagua Daniel Kalinaki wa Jukwaa la Wahariri Uganda kuwa Rais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki kuanzia Mei 12, 2023, ambapo ataongoza kwa mwaka mmoja.
Deodatus Balile, ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), naye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, kuanzia Mei, 2024 hadi Mei, 2025.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Balile anasubiri kushika wadhifa wa Urais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki mwezi Mei 2024, kwa sasa atakuwa ni Naibu Rais wa Jumuiya ya Wahariri ya Afrika Mashariki.
Umoja wa Wahariri wa Afrika Mashariki Katiba yake inatoa nafasi ya kumwandaa kiongozi wake ajaye kwa mwaka mmoja baada ya kumchagua kama sehemu ya maandalizi ya kuifahamu vyema kazi yake kabla ya kushika madaraka hayo rasmi.