Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson,ameitaka Serikali kupitia Wizara za Afya, TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Rais UTUMISHI kuangalia upya utaratibu wa utoaji wa ajira kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele kwa watu wanaojitolea kufanya kazi bila malipo katika nafasi hizo.

Dkt.Tulia ameyasema hayo wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa kumi na moja wa Bunge ukiendelea Bungeni Jijini Dodoma leo Aprili 6, 2023.

“Huwa haipendezi sana zinapotangazwa ajira mpya zinapotolewa unakuta wale watumishi wote waliokuwa wakijitolea katika nafasi hizo hakuna hata mmoja aliyepata. Sasa huwa tunajiuliza ni kwamba wale wanaojitolea hawana sifa na waliopo nyumbani ndio wanasifa zaidi?” amesisitiza Dkt.Tulia.

By Jamhuri