Na Byarugaba Innocent, JamhuriMedia, Kibaha

Jumla ya Miradi 15 yenye thamani ya bilioni 3,120,194,399.98 inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha utakapokimbizwa siku ya Alhamisi tarehe 2 Mei,2024

Mwenyekiti wa Sherehe za Mwenge Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon John amesema Kibaha Mji itapokea Mwenge wa Uhuru katika Kata ya Visiga viwanja vya shule ya Msingi Visiga ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha chini ya Kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”

Mradi wa Maji Shule ya Msingi Visiga

Aidha,Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Kilometa 45 kwenye Kata 7 za Visiga, Misugusugu, Kongowe,Mkuza,Picha ya Ndege,Tumbi na Mailimoja kati ya Kata 14 zinazounda Halmashauri ya Mji Kibaha.

Dkt.Rogers Shemwelekwa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha ameeleza kuwa Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru,2024 imetekelezwa kwa viwango vya juu vinavyosadifu thamani ya fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha Shilingi 1,168,850,600,fedha kutoka Halmashauri shilingi 635,049,999.98, fedha kutoka kwa Wahisani shilingi 410,032,500, nguvu za Wananchi shilingi 903,261,300 na Mchango wa Mwenge ikiwa ni shilingi 2,000,000.00

Mwenyekiti wa Sherehe za Mwenge Wilaya Mhe.Nickson Simon John ametoa rai kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu kuhudhuria na kuulaki Mwenge wa Uhuru,2024 kuanzia kwenye eneo la Mapokezi, kwenye Miradi yote itakayotembelewa na jioni kushiriki shamrashamra za Mkesha zitakazoendelea kwenye viwanja vya stendi ya zamani ya Mailimoja.

Madarasa mawili Shule ya Msingi Misugusugu
Kituo cha Afya Kongowe

By Jamhuri