Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Tarime

Mkuu wa Wilaya Tarime, Kanali Maulidi Hassan Surumbu amempongeza Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara kwa kubuni semina ya maendeleo ya matokeo ya sensa 2022 ambayo ilishirikisha watu zaidi ya 1600 kutoka makundi mbalimbali wakiwemo madiwani,watumishi na makatibu wa CCM.

Semina hiyo iliyofanyikia katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Tarime (TTC) Kanali Surumbu amesema Halmashauri ya Tarime Vijijini wanakusanya vizuri mapato kwani taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Solomon Shati Mkoani Mjini Musoma Aprili 29,2024 ilikuwa nzuri hivyo wazingatie zaidi ukusanyaji wa mapato na kuongeza kuwa kila mmoja kwa nafasi yake afanye kazi kwa kuzingatia ilani ya Chama.

Mkuu wa Wilaya yaTarime Kanali Mauridi Hassan Surumbu

Azuiya Watalamu kutosimamia miradi kwani wanaposimamia wanasabibisha miradi kutofanyika kwa ufanisi pamoja na kutokamilika kwa wakati na yeye hayuko tayari kuona miradi inafanyikia chini ya kiwango.

Aidha amewataka viongozi kushughulikia kero za wananchi kwa wakati, kushirikiana naye kwa kusimamia ulinzi wa amani na utulivu hususani kwenye maeneo ya mipaka na Nchi jirani ya Kenya sambamba na kukemea biashara ya madawa ya kulevya.

Mbunge Mwita Waitara ametumia nafasi hiyo kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan kura ya kuwa Rais 2025 kutokana na maendeleo mengi aliyoifanyia Halmashauri ya Vijijini na kuiomba Serikali kukarabati barabara zilizoharibika kufatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Mbunge Tarime Vijijini Mhe Mwita Waitara

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amewapatia mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victor ambao utanufaisha Wilaya ya Rorya, Tarime Vijijini pamoja na Tarime Mjini wenye thamani ya bilioni 138,amepata mradi wa barabara wenye thamani ya bilioni 34 ingawa bado unasua sua kwa sababu ya malipo bilioni 6 bado hazijakamilika barabara ambayo amesema itakuwa mkombozi.

Amesema wananchi wa Tarime Vijijini wanajitolea kwenye maendeleo na wanachangia elimu kwa sababu wanapenda elimu katika Jimbo lake amejenga shule nyingi kwa kushirikiana na Wananchi .

Waitara ambaye hakusita kuongelea fedha za CSR kwenye semina hiyo amesema ni uchu na uroho wa madaraka kwa wengine kutaka kunufaika peke yao na fedha hiyo inayotolewa na mgodi wa Barrick kwaajili ya huduma za Jamii.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daudi Ngicho amesema CCM ya sasa iko makini sana ndio maana miradi mingi imefanyika na kuongeza kuwa ilani ya Chama hicho haikuchaguliwa na WanaCCM peke yake bali na vyama vya upinzani vilishiriki kuipigia kura ndio maana CCM ilishinda kwa kishindo 2020 uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti CCM Wilaya ya Tarime Daudi Ngicho.

Amesema anejivunia kuwa na Rais Makini Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Yuko vizuri na anaamini Watanzania wanakiamini Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuongeza kuwa wao CCM wana Mgombea 2025 tofauti na vyama vya upinzani ambayo havijaandaa wagombea bali vinasumbiria CCM igawanyike ndio wapate Mgombea toka CCM jambo ambalo halitatokea.

Diwani wa Kata ya Nyamwaga Mhe Mwita Marwa Magige(Vatican) mmoja wa washiriki wa semina hiyo amewashukuru waandaaji wa semina hiyo ya watu na makazi kupitia Mtakwimu Mkuu Demogratius Malamsha na timu yake kutoa mafunzo hayo.

Amesema anashukuru kwa semina hiyo kwani kwa sasa wamejua idadi ya Watu walioko kwenye Jimbo la Tarime Vijijini pamoja na na kwenye kata zao .

“semina ilikuwa nzuri angalau sasa tumeweza kufahamu idadi ya wakazi wa Kata zetu katika kata yangu ya Nyamwaga sasa tutafanya mipango kwa kuzingatia idadi ya watu tulio nao” alisema Vatican