Habari za Kitaifa

Chuo cha sukari matatani

Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Sukari Tanzania (NSI) kilichopo Morogoro, umelalamikiwa kwa kukiendesha chuo kama taasisi binafsi. JAMHURI imepata taarifa kuwa chuo hicho hadi sasa kimeendeshwa kwa kipindi cha miaka tisa bila kuwa na Baraza la Uongozi. NSI inaongozwa na Kaimu Mkuu wa Chuo, Julius Raphael Deteba, na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Salumu Mwanalelo, ambao wamekuwa ndiyo wenye mamlaka ...

Read More »

2016: Mwaka wa machungu kwa ‘mapedejee’

Zikiwa zimesalia siku 18 tu kumaliza kwa mwaka huu, baadhi ya Watanzania wameuona mchungu katika Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli. Mwaka huu umekuwa mchungu kwa wale waliozoea kuishi kwa mipango, wasiokuwa na kazi maalumu zaidi ya kuishi maisha ya ujanjaujanja, huku wakiwa na matumizi makubwa ya pesa. Ni mwaka ambao kila mmoja alikuwa na mipango. Kuna ...

Read More »

MSCL kitendawili kigumu

Baada ya miezi 10 bila ya wafanyakazi wa MSCL kupata mishahara, Serikali imeonekana kutaka kutekeleza ahadi yake ya kutaka kuifufua Kampuni hii. Serikali imefanya mabadiliko ya uongozi katika baadhi ya nafasi kwenye menejimenti, imekaribisha na inashindanisha makampuni mawili ya kigeni kwa lengo la kufanya ukarabati mkubwa kwenye baadhi ya meli na inakusudia kutekeleza mradi wa ujenzi wa meli mpya katika ...

Read More »

Kilichomng’oa bosi Jeshi la Magereza

Aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja, hakuomba kujiuzulu kwa ridhaa yake, JAMHURI limethibitishiwa. Badala yake, kiongozi huyo amefikia hatua hiyo baada ya kuwapo tuhuma kadhaa za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili. “Ziara ya ghafla ya Rais John Magufuli, pale Ukonga haikuwa ya bahati mbaya. Alijua nini anachokwenda kukifanya maana tayari taarifa zote zinazomhusu Minja, alishakuwanazo,” kimesema ...

Read More »

Bomu la Dangote

Wakati joto likizidi kupanda kuhusu hatma ya kiwanda cha saruji cha Dangote kilichoko Mkoani Mtwara, JAMHURI limebaini kuna mgogoro mkubwa wa uongozi ndani ya kiwanda hicho, lawama zikielekezwa kwa serikali. Mmoja wa maafisa wa kampuni ya Dangote, ambaye amezungumza na JAMHURI kwa masharti ya kutotajwa gazetini, amesema yapo mambo ambayo hayakubaliki yanayofanywa uongozi wa kiwanda hicho cha kuzalisha saruji. Amesema ...

Read More »

Watumishi Wizara ya Ardhi wapora ardhi

Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wanatuhumiwa kutumia nyadhifa zao kupora shamba la hekari 74.2 mali ya Mwenegowa Mwichumu mkazi wa Kibada Kigamboni Dar es salaam. Kabla ya uporaji huo shamba hilo lililokuwa na miti ya minazi, michungwa pamoja na miti mingine ambayo imeharibiwa na watu hao waliojimilikisha eneo hilo bila ya kufuata taratibu ...

Read More »

Prof. Ndalichako amvaa Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameingia katika mapambano ya wazi na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako kwa kumpa maagizo, ambayo ameyakataa. Makonda amemwagiza Waziri Prof. Ndalichako asiwasikilize wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Al-Muntazir iliyopo jijini Dar es Salaam, lakini kinyume chake, Prof. Ndalichako ameunda Kamati ya kuchunguza malalamiko ya ...

Read More »

Unyayasaji kingono washika kasi Kilimanjaro

Matukio ya watoto  kunyanyaswa kingono katika mji wa Moshi, yameibuka kwa kasi ya kutisha  na kutishia usalama wa watoto, huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa shule za msingi. Udhalilishaji huo unatokea huku wazazi wakitupiwa lawama kwa kushindwa kutoa ushirikiano vya vyombo vya dola watoto wao wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia, ikiwamo kubakwa na kulawitiwa. Kwa mujibu wa taarifa ya mashirika ...

Read More »

Uchumi unakuwa kwa matabaka

Wakati Rais John Magufuli akieleza kuwa uchumi wa nchi umekuwa kwa asilimia 7.9 hadi kufikia robo ya mwaka huu na kuifanya Tanzania kushika nafasi ya pili baada ya Ivory Coast, Mchumi Mwandamizi na Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi, amesema uchumi umekuwa kwa matabaka. Profesa Ngowi ameieleza JAMHURI, kuwa ukuaji wa uchumi unaoelezwa wakati mzunguko ...

Read More »

Rais Magufuli ajaribiwa

Hatua ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuwafutia mashitaka ya ujangili watu tisa, wakiwamo wenye nasaba na Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla; imeibua ‘kilio’ miongoni mwa watu walio katika mapambano dhidi ya ujangili nchini. Kuachiwa huru kwa watuhumiwa hao kunaelezwa kuwa ni jaribio kubwa kwa uongozi wa Rais John Magufuli, ambaye ameapa kupambana ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 22

Barabara ya Bagamoyo balaa   UCHAMBUZI WA KINA  453. Barabara za New Bagamoyo na Pugu-Chanika-Mbagala ndizo ambazo zimethibitika kuhusisha sana matatizo makubwa ya ukikwaji wa taratibu na maadili mema ya kazi.   454. New Bagamoyo Road  (a)  Urefu: Kilometa 13.4 kuanzia makutano ya Barabara ya Sam Nujoma hadi njia panda ya kuelekea Kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill.   (b) ...

Read More »

Katibu wa Nyerere ‘afa’ njaa

Paulo Sozigwa, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu wa Rais Julius Kambarage Nyerere, anakabiliwa na hali ngumu kimaisha. Sozigwa, ambaye kwa sasa anaumwa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer), anaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu, akisaidiwa na familia yake na wasamaria wema.  Kutaabika huko kumechangiwa na kutopata malipo ya kiinua mgongo na pensheni, kwa kile kinachoelezwa kwamba ...

Read More »

YUTONG yazindua basi la kisasa

Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong kwa kushirikiana na Benbros Motors Ltd, imezindua basi la kisasa lenye uwezo mkubwa ili kupunguza ajali za mara kwa mara. Akizungumza katika uzinduzi huo, Afisa Masoko, Albert Currussa, wa Benbros Motors Ltd anasema kwamba kampuni hiyo imeingiza sokoni gari hilo F12Plus lenye uwezo wa kuhimili barabara za aina zote. Albert anasema kwamba basi ...

Read More »

Kodi kikwazo cha uchumi

Serikali imetakiwa kuboresha mipangilio ya ulipaji kodi ikiwamo kuondoa tozo zisizokuwa za ulazima, ili kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji pamoja na kuepuka kupungua kwa mzunguko wa fedha. Akifanya mahojiano maalumu na JAMHURI, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, Professa Prosper Ngowi, anasema kukosekana kwa fedha katika mzunguko kunatokana na mpangilio wa sera za ulipaji kodi. Prof. Ngowi ambaye ...

Read More »

Bunduki 13 zanaswa familia ya Mbunge

Watu kadhaa, wakiwamo wenye nasaba na Mbunge wa Mbarali, mkoani Mbeya, Haroon Mulla (CCM), wamekamatwa katika operesheni maalumu wakituhumiwa kujihusisha na ujangili. Katika operesheni hiyo, inayoongozwa na kikosi kazi kinachovishirikisha vikosi vya ulinzi na usalama, bunduki 13 za aina mbalimbali zimekamatwa kwa ndugu zake Mulla. Mtoto wa Mulla, anayetajwa kwa jina la Fahad, ni miongoni mwa waliokamatwa na idadi kubwa ...

Read More »

Kiwanda cha Bakhresa chachafua mazingira

Maisha ya wananchi wanaoishi jirani na Kiwanda cha Bakhresa cha kuchakata matunda kilichopo katika Kijiji cha Mwandege, Mkoa wa Pwani, yapo hatarini kutokana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati tofauti, wananchi hao wanasema maisha yao yapo hatarini kutokana na mfumo wa majitaka unaotiririsha maji kutoka ndani ya kiwanda hicho na kutiririshwa kwenye makazi yao. ...

Read More »

Waajiriwa Uhamiaji bila kupewa barua

Ikiwa ni mwezi wa tano sasa vijana 300 walioajiriwa katika Idara ya Uhamiaji wakiwa hawajalipwa mishahara, imebainika kuwa chanzo ni kutopewa barua zao za ajira. Rais John Magufuli, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu, Dar es Salaam wiki iliyopita, alisema askari polisi na wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama walioajiriwa hivi karibuni wamekuwa wakilipwa mishahara. Hata hivyo, ...

Read More »

Polisi ‘mwizi wa magari’ afukuzwa kazi

Jeshi la Polisi limemfukuza kazi askari wake, PC Hamad Mud wa Kituo cha Polisi Sanya Juu, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, akitajwa kuwa kinara wa mtandao wa wizi wa magari. Kwa uamuzi huo, Mud anasakwa ndani na nje ya nchi ili afikishwe mahakamani. Amekuwa akihusishwa na wizi wa magari kutoka Kenya, Rwanda na Uganda. Anatajwa kuwa na uhusiano mkubwa na maofisa wa polisi ...

Read More »

Malipo Polisi utata

Ikiwa ni miezi mitatu tangu Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Frank Msaki, asimamishwe kazi kutokana na tuhuma za kufanya malipo hewa ya posho za chakula kwa askari, JAMHURI imebaini yaliyojificha nyuma ya sakata hilo. Tuhuma hizo zilimsukuma Rais, Dk. John Magufuli kuagiza kuondolewa kwa watumishi raia katika majeshi ya ulinzi na usalama nchini, jambo ambalo tayari limeshaanza kutekelezwa na ...

Read More »

Polisi Dar lawamani

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeshiriki katika kuingia kwa mabavu katika eneo la biashara la kampuni ya uuzaji mafuta ya Petrofuel (T) Limited na Isa Limited, hali ambayo ni kinyume cha utaratibu. Askari Polisi, waliotumika kuingia katika eneo hilo ni wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), katika eneo linalosadikiwa kuwa na ugomvi wa kibiashara. Pamoja ...

Read More »

Chuo Kikuu Huria kwafukuta

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dk.Hamza Kondo amesimamishwa kazi ya uhadhiri katika mazingira ambayo ameyataja kujaa utata na ukiukwaji wa taratibu za utumishi. Akizungumza na JAMHURI, Dk. Kondo ambaye amekuwa mhadhiri katika kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii, Idara ya Uandishi wa Habari kwa miaka kadhaa, katika kipindi amefanya kazi kama mkuu wa idara hiyo. Mhadhiri huyo ...

Read More »

Kiwanda cha Polyester chawaliza wafanyakazi

Waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Morogoro Polyester Textile cha mjini Morogoro, wameiomba Serikali kuingilia kati ili waweze kulipwa madai yao baada ya kuachishwa kazi miaka 18 iliyopita. Akizungumza na JAMHURI, Laurian Kazimilli, Mwenyekiti wa wastaafu hao, anasema miaka 18 imepita tangu waanze kuhangaikia madai yao na kuna wenzao wengi ambao tayari wametangulia mbele ya haki. Anasema idadi kamili ya ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons