Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,Arusha

Tanzania imekua na maendeleo makubwa ya huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu mijini na vijijini kwa kufanikisha laini za simu milioni 72.5 Machi mwaka huu kutoka laini milioni 64.1 za Juni mwaka 2023 .

Katika kipindi hicho idadi ya watumiaji wa mitandao ya intaneti imekua hadi kufikia watu milioni 36.8

Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehama.

“Idadi kubwa ya Watanzania wa mijini na vijijini imefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu na mitandao ya Internet, haya ni maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini,”.

Amesema idadi hiyo ni kubwa kufikiwa katika utoaji wa huduma hizo, ukilinganisha na nchi zingine huku upatikanaji wa huduma hizo kumewezesha jamii ya watanzania kushirikia ipasavyo uchumi wa kidijiti.

Pia ameagiza vyuo vikuu,ya kati,shule za sekondari na Msingi kuanzisha klabu za kidijiti ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi na kukuza ujuzi wa kidijiti.

“Tutoe matukio zaidi kwa watoto wa kike ili wapende kusoma masomo ya sayansi ili wasiwe wababaishaji na mambo yao yataenda vizuri lakini pia utumiaji wa Tehama utawezesha kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa”

By Jamhuri