Aprili 25, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Tabora, mbele ya Demetrio Nyakunga, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba ECC. 10892/ 2024 ya Jamhuri dhidi ya Bw. Michael Fredrick Mgongo Mhadhiri katika Chuo Cha Utumishi wa Umma (TPSC) Tawi la Tabora.

Mwendesha Mashtaka kutoka TAKUKURU Mwanaidi Mbuguni ameieleza Mahakama kwamba mshtakiwa aliomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (Uhazili) ili amfanyie upendeleo na kumfaulisha masomo aliyofeli.

Mshtakiwa alisomewa mashtaka yanayomkabili na kukana mashtaka hayo.

Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na yuko nje kwa dhamana ambapo kesi hiyo itakuja tena Mei 23,2024 kwa ajili ya kusoma hoja za awali kwa mshtakiwa na kuanza kusikilizwa kwa upande wa Jamhuri.

By Jamhuri