1. Falme za Kiarabu

Nafasi ya kwanza inashika na falme za kiarabu ambapo kuna jengo lefu kuliko yote duniani ambalo lipo kwenye jiji Dubai na Linaitwa Burj Khalifa.

2. China

Nafasi ya pili inashika na China ambapo kuna jengo lefu linaitwa Shanghai Tower

linaloshika nafasi ya pili kwa urefu duniani ambalo linapatika katika jiji la Shanghai China na lina urefu wa mita 632 (ghorofa 128) kutoka uso wa ardhi. Lilijengwa mwaka 2015 .

3. Saudi Arabia

Nafasi ya tatu inashika na Saudi Arabia ambapo kuna jengo lefu linaitwa Abraj AL-Bait clock Tower linaloshika nafasi ya tatu kwa urefu duniani ambalo Linapatikana katika mji mtakatifu kwa Waislamu wa Mecca nchini Saudi Arabia.

Lilijengwa mwaka 2012 na linashikilia rekodi ya kuwa mnara wa saa mrefu zaidi duniani sanjari na kuwa hoteli ndefu zaidi duniani.

4. Korea Kusini

Korea Kusini kunapitkana jengo refu lina urefu wa mita 555 (ghorofa 123) na lilikamilika mwaka 2016 na linaitwa Lotte world tower lipo katika jiji kuu la Korea Kusini la Seoul.

5. Marekani

Marekani kuna jengo linaitwa One world Trade Centre ambalo linapatikana katika jiji la kibiashara la New York nchini Marekani. Lina urefu wa mita 514 (ghorofa 104) na lilijengwa mwaka 2014.

Jengo hili linafahamika pia kama the “Freedom tower” limejengwa jirani na jengo la World Trade Centre lililoshambuliwa na magaidi September 11 mwaka 2001.

6.Taiwan

hapa lipo jengo la Taipei 101 linashika nafasi ya nane kwa urefu wa majengo duniani likiwa na urefu wa mita 509 pamoja na ghorofa 101. Lilijengwa mwaka 2004 na tangu mwaka huo hadi mwaka 2010 lilikua ndiyo jengo refu zaidi duniani kabla rekodi hii haijavunjwa na Burj Khalifa.

Linasifika kwa kuwa jengo kubwa na refu zaidi duniani lenye miundombinu rafiki kwa mazingira (the tallest and largest green building in the World). Linapatikana katika jiji la Taipei nchini Taiwan barani Asia.

By Jamhuri