Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewasili jioni ya tarehe 20 Aprili 2024, Jijini Nairobi, Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Kenya (CDF), Jenerali Francis Ogolla aliyefariki kwa ajali ya Helikopta tarehe 18 Aprili 2024, Kaben Marakwet Mashariki mwa Kenya.

Katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jijini Nairobi Mhe. Dkt. Biteko alipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki anaeshughulikia Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, akiambatana na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Tanzania, Wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Please follow and like us:
Pin Share