Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro amefariki dunia leo Ijumaa Aprili 27, 2018 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Awali alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kabla ya kustaafu utumishi wake, Kandoro alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambapo alipokelewa kijini ya Amos Makalla.

Mpaka kustaafu kwake, Abbas Kandoro alikuwa ameshika nafasi ya ukuu wa mikoa katika zaidi ya mikoa sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.

 

1677 Total Views 1 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!