Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii imepitishwa hivi leo bungeni ikiwa na mikakati madhubuti ya kuendeleza, kuimarisha shughuli za Uhifadhi na Utalii.

Akijibu hoja za Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii,Mohamed Mchengerwa (MB) alisema

“Niwahakikishie wabunge nitajenga matumaini, ninatambua kila mbunge ameongea kuhusu changamoto zilizopo. Naahidi nitaingia katika mioyo yenu nikibeba changamoto zote mlizotoa na kuzishughulikia kwa maslahi ya wananchi”.

Aliongeza kuwa wakati ni sasa kama Wizara tutafanya yote mliyo elekeza kumaliza changamoto ili wakati mwingine tuongelee maendeleo ya Utalii na sio changamoto.

Pia, Waziri Mchengerwa ameweza kutoa ofa kwa timu ya Yanga (wananchi) kutembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na Ngorongoro na kubainisha safari hiyo itaitwa “The CAF Finalist Royal Tour” kwa tarehe itakayopangwa.

Aidha,alisisitiza viongozi wa Taasisi kufanya kazi kwa weledi kwa kumaliza migorogo ya wanyama wakali wanaoingia katika maeneo ya wananchi.

Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akichangia amesema tayari nuru imeshaanza kuonekana kwa ushirikiano walioonyesha wabunge katika uchangiaji wao wa changamoto nyingi zilizopo katika Wizara.

“Pongezi kwa wabunge kwa kutuonyesha njia na namna ya kwenda tumepokea ushauri, maelekezo, mapendekezo, maoni tunaahidi tutayafanyia kazi”.

Vile vile, tutashuka chini na kuongea na wananchi na kujadili nao matatizo yao na kuyafanyia kazi ili migogoro iishe.

By Jamhuri