Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Askofu Mkuu wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni jijini Dar es Salaam, Bishop Rose Mgeta amesema Kanisa hilo litaendelea kutekeleza maono ya Mwanzilishi wa Kanisa hilo, Hayati Askofu Dk Getrude Rwakatare kutimiza maono yake kama kuendeleza makongamano ya uamsho wa ndoa kila mwaka.

Hayati Dk. Getrude Rwakatare alianzisha kongamano la uamsho wa ndoa mwaka 2000 kwa lengo la kuhakikisha anaokoa ndoa nyingi baada ya kuona ndoa nyingi zikiingia kwenye mogogoro na kusababisha watoto wengi kuachwa mitaani.

Bishop Rose Mgeta akizungumza kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki na Maaskofu waliohudhuria hafla hiyo ni Rose Mgeta wa Mlima wa moto, Dastan Maboya, Richard Hananja, Daniel Mgogo,

Askofu Rose amesema kupitia tukio la uamsho wa ndoa, ndoa nyingi zimepona kutokana na shuduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watu waliokuwa wanahudhuria makongamano hayo.

Amesema hata watoto wa hayati Getrude Rwakatare wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ndoto za mwanzilishi wa Kanisa hilo zinatimizwa.

Mtoto wa Hayati Dr Getrude Rwakatare, Dk. Rose Rwakatare, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, alisema kongamano la uamsho wa ndoa ilianzishwa mwaka 2,000 kupitia maono ya mwanzilishi wa Kanisa la Mlima wa Moto, Hayati Getrude Rwakatare.

Amesema kutokana na huduma kubwa ambayo Mungu alimkirimia kuhudumia waumini wa Kanisa na katika huduma zote Mungu alizomwitia katika ndoa alitilia mkazo watu kupendana na kuheshimiana na ndipo akaanzisha uamsho wa ndoa.

“Askofu Rwakatare alipenda wanandoa waishi kwa upendo ili ndoa ziweze kudumu na kuwa bora na zilizojaa amani na utulivu kwani hapo ndipo afya ya akili inapokuwepo na kuwa na familia bora,” amesema.

Wageni mbalimbali wakipata chakula kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Dk. Rose alisema kwa kushirikiana na wazee wa Kanisa hilo na askofu wa kanisa hilo, Askofu Rose Mgeta wamefanikisha kuendeleza tukio la uamsho wa ndoa kwa miaka yote na kwamba wamekusanyika kufanya uamsho wa ndoa ili ziweze kupata uamsho na ndoa ziweze kupona na kuwapa amani ya moyo wana ndoa.

“Kuwa na ndoa yenye masilikilizano inawezekana, Biblia inasema utaacha wazazi wako utaambanana na mwenzako na mtakuwa mwili mmoja sasa mwanaume asimame kwenye nafasi yake na mwanamke naye asimame kwenye nafasi yake kama mama na hapo mtayashinda majaribu yote.

“Jambo hili linasaidia kuwakumbusha wanandoa kuhusu mambo ambayo yako kinyume na mila na desturi za kitanzania kama mambo ya kuiga yanayoleta mmomonyoko wa maadili kwenye taifa, mfano ukatili wa majumbani unaosabaaisha vifo, kila kukicha unasikia huyu kampiga risasi mwenzake, huku kamchinja mwenzake haya hayakubaliki,” amesema.

Aidha, Dk.Rose amesema wimbi jipya linaitesa dunia ni ndoa za jinsia moja na yeye kama Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro amekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo kwani havitaleta mustakabali mwema kwa taifa la Tanzania.

“Tumuunge mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan, hili ni pepo ambalo tunapaswa kulikemea kwa nguvu zetu zote, tunapaswa kusali kwa bidii ili liondoke, kama majanga mengine ambayo tulipiga magoti yakaondoka hili nalo kwanini tusiombe likaondoka, wazazi tusimame kwa umoja wetu kupinga jambo hili, “ amesema

Mchungaji aliyejipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii, Richard Hananja akifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Kwa upande wake, Askofu Daniel Mgogo amesema amekuwa akitoa mafundisho mbalimbali ya ndoa kwenye mitandao ya kijamii lakini kwa muda wa miezi sita hakuandika chochote kwani alikwua nchini Marekani.

“Kumbe yale mafundisho yangu mnayapenda kwasababu nimekuta watu wengi wameniandikia kwenye mitandao yangu ya kijamii kwamba mbona hatuyaoni, lakini kwenye uamsho wa ndoa sitapiga nondo,” amesema.

“Katika viumbe ambavyo vinahitaji ustadi wa hali ya juu kukaa navyo ni binadamu, kukaaa na kiumbe kinaitwa binadamu ni kazi kubwa sana hata wachungaji kuchunga watu wanaitwa binadamu mwaka mzima ni kazi kubwa sana na inabidi ukifikisha mwaka upate muda wa kupumzika maana ni kazi kubwa,” amesema.

Washiriki mbalimbali wakifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Askofu Danstan Maboya akifanya maombi kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Wageni waalikwa wakifuatilia kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

By Jamhuri