Na Mwandishi Wetu, JakhuriMedia, Dodoma

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola imefanikisha kukamata jumla ya kilogramu milioni 1.96 za dawa za kulevya mwaka 2023.

Katika ukamataji huo, watuhumiwa 10,522 kati yao wanaume 9,701 na wanawake 821 walikamatwa na Mamlaka hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akipokea Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya Nchini kwa mwaka 2023 kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo (Kulia) katika Ukumbi wa Habari Bungeni tarehe 16 Mei 2024 Jijini Dodoma

Katika taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema dawa za kulevya zilizokamatwa ni Heroin kilogramu 1,314.28, Cocaine kilogramu 3.04, na methamphetamine kilogramu 2,410.82.

Nyingine ni bangi kilogramu 1,758,453.58, mirungi kilogramu 202,737.51, Skanka kilogramu 423.54 na dawa tiba zenye asili ya kulevya gramu 1,956.9 na mililita 61,672.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya Nchini kwa mwaka 2023 kwa waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Bungeni tarehe 16 Mei 2024 Jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) Aretas Lyimo akifafanua jambo kuhusu Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya Nchini kwa mwaka 2023 katika Ukumbi wa Habari Bungeni tarehe 16 Mei 2024 Jijini Dodoma.