Na Peter Haule,JamhuriMedia,Singida

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewataka wananchi wote ambao hawajafikiwa na zoezi la sensa kuendelea kutenga muda na pia wakifikiwa watoe ushirikiano kwa makarani wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi

Dkt.Nchemba ameyasema hayo kijijini kwake Misigiri Kiomboi Iramba mkoani Singida baada ya kuhesabiwa wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi lililoanza rasmi leo Agosti 23 nchini kote.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia) akiuliza jambo kwa watu waliopo katika makazi yake (hawapo pichani), wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi, kijijini kwake Misigiri Kiomboi Iramba Mkoani Singida.

Amesema kuwa ni vema wananchi wote wakatoa taarifa zikiwemo za makundi maalumu wakiwemo walemavu ili taarifa hizo ziweze kumsaidia Mhe. Rais katika masuala ya kupanga mipango ya maendeleo na utekelezaji wa bajeti.

Dkt. Nchemba amesema kuwa amefurahia zoezi la Sensa kwa kuwa maswali yote aliyoulizwa hayakuwa na utata bali yalikuwa ya maendeleo.

Alisema kuwa karani amekuja kwa wakati na ametumia utaratibu uliozingatia maandalizi ya sensa ya watu na makazi yaliyofanyika

By Jamhuri