Daily Archives: September 3, 2019

CWT inavyopigwa

Maji yanazidi kuchemka ndani ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT), huku mkataba wa kinyonyaji wa mshauri wa mradi wa ujenzi na madeni kwenye Mfuko wa Jamii wa PSPF, yakiwa ni miongoni mwa mambo yanayoendelea kwenye chama hicho.  JAMHURI limebaini CWT iliingia mkataba wa kinyonyaji na Kampuni ya Settlements De Popolo Consultants wenye gharama ya Sh milioni 960, lakini kutokana na ...

Read More »

‘Tumeuza kila tulichonacho, hatuwezi kutoka Muhimbili’

Mkazi wa Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma, Sijawa Jafar, mwenye umri wa miaka 35 ameiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia kulipia gharama za matibabu ya mumewe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinazofikia Sh milioni 3.7, baada ya familia hiyo kushindwa kupata fedha hizo. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, Sijawa ameiomba serikali na wadau mbalimbali kumsaidia kulipa gharama hizo ...

Read More »

Serikali yazinduka matrekta mabovu

Na Deodatus Balile Baada ya Gazeti la JAMHURI kuchapisha habari za ubovu wa matrekta ya URSUS yanayouzwa kwa wakulima nchini kutoka Poland, Bunge limeibana serikali, ambayo nayo imezinduka na kuchukua hatua, JAMHURI linathibitisha. Kampuni ya URSUS S. A. iliingia mkataba na Shirika la SUMA JKT siku nane kabla ya uchaguzi mkuu, yaani Oktoba 22, 2015 kwa nia ya kuzalisha na ...

Read More »

‘Trafiki’ Dar wanatosha

Wakati Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, akifikiri kuongeza idadi ya askari wa usalama barabarani, mamlaka ndani ya Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inao askari hao wa kutosha. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Marison Mwakyoma, anayeshughulika na suala la usalama barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, amesema kitengo hicho kwenye eneo lake ...

Read More »

TRAWU wafukuzana Dar

Wanachama wa matawi matano wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) wamekutana jijini Dar es Salaam na kuunga mkono uamuzi wa Kamati Maalumu ya Dharura wa kuwasimamisha kazi viongozi wa kitaifa wa chama hicho. Hatua hii imetokana na mgogoro ulioanza baada ya uongozi wa TRAWU kupindua mapendekezo ya wanachama siku ya Mei Mosi, 2019, ambapo mtumishi waliyemchagua awe mfanyakazi ...

Read More »

Matrekta ya URSUS yadhibitiwe

Kwa wiki tatu mfululizo tumekuwa tukiandika habari juu ya mkataba wa kununua matrekta na kujenga kiwanda cha kuunganisha matrekta cha URSUS kilichopo wilayani Kibaha. Kiwanda cha kuunganisha matrekta kwa mujibu wa mkataba ilibidi kiwe kimekamilika Juni, mwaka jana. Hadi leo kazi iliyofanyika ni ndogo kwa kiwango kisichoridhisha. Kampuni ya URSUS iliingia mkataba na SUMA JKT, ambayo baadaye imehamishia mkataba huu ...

Read More »

NINA‌ ‌NDOTO‌ ‌(33)‌

Nitawezaje‌ ‌kuamka‌ ‌mapema?‌ ‌ “Ni‌ ‌jambo‌ ‌la‌ ‌aibu,‌ ‌ndege‌ ‌wa‌ ‌angani‌ ‌waamke‌ ‌kabla‌ ‌yako,”‌ ‌alisema‌ ‌Abu‌ ‌Bakr,‌ ‌rafiki‌ ‌wa‌ ‌karibu‌ ‌sana‌ ‌wa‌ Mtume‌ ‌Muhammad.‌ ‌ Siku‌ ‌moja‌ ‌wakati‌ ‌natazama‌ ‌video‌ ‌katika‌ ‌mtandao‌ ‌wa‌ ‌Youtube‌ ‌nilikuta‌ ‌video‌ ‌iliyokuwa‌ ‌ikimuonyesha‌ bondia‌ ‌maarufu‌ ‌Floyd‌ ‌Mayweather.‌ ‌Video‌ ‌hiyo‌ ‌ilimwonyesha‌ ‌akifanya‌ ‌mazoezi‌ ‌kando‌ ‌ya‌ ‌bahari‌ ‌saa‌ 10 alfajiri.‌ ‌Baada‌ ‌ya‌ ‌kuulizwa‌ ‌kwanini‌ ‌anafanya‌‌hivyo‌ ‌alijibu,‌ ‌“Wenzangu‌ ...

Read More »

Wapandishwa kizimbani kwa kuiba bil. 1.4/-

Watu wawili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu ya kula njama na kuvamia, kuvunja makazi na kuiba fedha na vitu vyenye thamani ya Sh bilioni 1.4. John Masatu (45) na Phinias Mang’ara (47) wamefikishwa mahakamani hapo kwa kuiba kinyume cha kifungu cha 258 na 265 vya Sheria ya ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (27)

Wiki tatu zilizopita nilihitimisha makala hii katika sehemu ya 26. Nilieleza nani analipa VAT, utaratibu wa kujisajili, tarehe za kulipa VAT na taratibu nyingine. Nikiri kuwa nimekabiliwa na majukumu mengi ya kitaifa, ikiwamo kuchunguza matreka ya URSUS yanayowatia hasara wakulima. Niombe radhi kuwa sikuandika mada hii kwa wiki mbili zilizopita na nimekuwa nikipokea simu nyingi za kuuliza kulikoni. Sitanii, leo ...

Read More »

Maendeleo Bukombe yanavyokimbia (2)

Na angela kiwia Mbunge wa Bukombe, Dotto Biteko, katika mahojiano maalumu na JAMHURI kuhusu mambo ya maendeleo yanayoendelea jimboni kwake, amesema katika kipindi cha miaka mitatu mtazamo wa wananchi wa Bukombe umebadilika, tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Madini, amesema wananchi wamekuwa na mwamko mpya wa maendeleo, jambo ambalo linasaidia kubadilisha taswira ya jimbo na Wilaya ...

Read More »

Bandari za Mwanza kupaisha uchumi Maziwa Makuu

Katika makala hii tutaangazia miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa bandari zinazosimamiwa na Bandari ya Mwanza ndani ya Ziwa Victoria. Katika Ziwa Victoria, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inamiliki na kusimamia bandari kubwa za Mwanza Kaskazini, Mwanza Kusini, Nansio, Kemondo Bay, Bukoba na Musoma. Pia kuna bandari nyingine ndogo ndogo (Cluster Ports) ambazo ziko ...

Read More »

Ndugu Rais maisha haya mpaka lini?

Ndugu Rais, alianza waziri akasema ameshangaa kuona baadhi ya Watanzania wakishangilia kuzuiwa kwa ndege ya ATCL nchini Afrika Kusini. Hajawahi kuona sherehe msibani. Ashibae hamjui mwenye njaa – lazima ashangae. Inapotokea hata Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally, naye ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya Watanzania kufurahia kukamatwa ndege ya serikali inayotumiwa na ATCL, hapo lipo tatizo. Hakuishia hapo, akaongeza ...

Read More »

Tusipotoshe kauli tukaiharibu nchi (2)

Sehemu iliyopita, mwandishi wa makala hii alinukuu maneno kutoka kwenye kitabu kilichoandikwa na Mohammed Said, yaliyohusu hofu aliyokuwa nayo mmoja wa wana TANU, Sheikh Takadir, juu ya TANU kumezwa na Ukristo. Endelea… Hapo waweza kuona mbegu ya uhasama wa kidini ilipokuwa inaibuliwa. Lakini mwandishi Mohammed Said katika uk. 246 anaendelea kutuandikia hivi; “… It was at the TANU old office as we ...

Read More »

Nini maana ya utumishi wa umma?

Tukio la hivi karibuni limenisukuma kutafakari ni nini maana nzuri ya utumishi wa umma, na ni nini unapaswa kuwa uhusiano wa mtumishi wa umma na jamii yake. Kwenye hoja yangu najumuisha watumishi wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa kwa sababu, aghalabu, cheo kinawainua na kuwapa hadhi na mamlaka yaliyo juu ya wapiga kura na walipa kodi. Wote hawa nitawaita watumishi wa ...

Read More »

Kwanini Bageni anyongwe peke yake kati ya watu 13? (2)

Toleo lililopita tuliishia aya inayosema: “Kwa msingi huu, Mahakama Kuu haikumuona Bageni akifyatua risasi, kwa sababu si yeye aliyefyatua risasi, hivyo upande huo akaondolewa, lakini pia haikumuona akiamrisha risasi kufyatuliwa, kwa sababu aliyefyatua hakuwapo mahakamani kumtaja kuwa ndiye akiyemwamrisha kufyataua, hivyo upande huo nako akaondolewa. Mwisho akaonekana haingii popote kwenye kosa, basi akachiliwa huru.” Sasa endelea… Mahakama ya Rufaa Mahakama ...

Read More »

Ukipoteza muda, muda utakupoteza zaidi (2)

Wiki iliyopita makala hii iliishia pale ambapo ilikuwa inasomeka: ‘hauwezi ukashinda kama hauchezi, mwanadamu anaishi mara moja tu hapa duniani. Tunaloweza kulifanya sasa, tulifanye kwa sababu hatuishi mara ya pili hapa duniani. Kubahatika kuishi duniani ni fursa.’ Endelea… Ni fursa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, hatujapata fursa ya kuishi duniani kwa bahati mbaya. Mungu habahatishi. Mwanasayansi Albert anasema: “Mungu hachezi bahati nasibu.” ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (44)

Maneno ‘asante sana’ yanaroga mtoaji atoe zaidi Shukrani ni mtihani. Kwa mtazamo wangu, shukrani ni utajiri, kutoshukuru ni umaskini. Shukrani ni furaha, kutoshukuru ni huzuni. Shukrani ni fadhila, kutoshukuru ni kilema. Shukrani ni chanya, kutoshukuru ni hasi. Shukrani ni kicheko, kutoshukuru ni kilio.  Shukrani ni ongezeko, kutoshukuru ni upungufu. Shukrani ni nguvu, kutoshukuru ni udhaifu. Shukrani ni kujipenda, kutoshukuru ni ...

Read More »

Kauli za viongozi ziwe za hadhari, zisilete mauaji

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bashiru Ally, alipowataja wakuu wa mikoa wawili kuwa wamo kwenye orodha ya viongozi vijana watakaopelekwa kupata mafunzo ya uongozi, wapo ambao hawakumwelewa. Siku mbili baadaye, hao waliokuwa hawamwelewi, walimwelewa vizuri. Kati ya wakuu wa mikoa wawili waliotajwa, mmoja – yule wa Mkoa wa Mbeya – akaibuka na kauli chafu akihamasisha mauaji. Je, bado ...

Read More »

Mwana msekwa ndo mwana

Wazaramo ni miongoni mwa makabila zaidi ya 125 yanayofahamika na kuunda taifa la Watanzania. Ni wakazi wenyeji wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kiasili wana utamaduni wao na lugha mama mwanana – Kizaramo. Kihistoria na kijiografia wana ndugu zao kiasili ambao ni Wakwere, Wadoe, Wamashomvi, Waluguru na Wakutu. Lakini kwa mbali wanao Wazigua na Wabondei. Wazaramo wanao watani wao ...

Read More »

Yah: Mabango ya waganga wa kienyeji

Leo nimeamua kutotaka salamu wala kusalimia mtu, nimeamka na hili la mabango ya waganga wenye vibali vya kujitangaza kutibu magonjwa yaliyoshindikana hospitalaini na makanisani. Hata sielewi ni nani hasa ambaye anaweza akawajibika kwana kesi hii siku ya mwisho pale palapanda itakapolia huko mawinguni na akalakiwa na kupelekwa motoni kwa kuacha dhambi kubwa kama hii ikiendelea kutendeka mbele ya macho yake ...

Read More »

Sipendi kiki, kazi inanitambulisha Foby

Mwanamuziki anayetamba na kibao cha ‘Twende’, alichomshirikisha Barnaba Classic kinachoshika chati ya juu katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni, Frank Ngumbuchi, maarufu Foby, amesema hana mpango wa kujiingiza kwenye ‘kiki’ zisizokuwa na maana. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI kuhusu kazi zake za sanaa, Foby amesema alianza kutambua kwamba ana talanta ya muziki mwaka 2012 wakati akiwa anasoma katika Shule ...

Read More »

Kudumu Ligi Kuu uwe roho ngumu

Siku zote wachezaji wavivu ndio wanapenda kulalamika mno uwanjani. Kauli kama hii iliwahi kusikika: “Aaah! Ticha inatosha bwana, kwa leo inatosha.” Huyo ni mchezaji wa zamani wa Yanga akimwambia kocha wake kuwa muda wa mazoezi umekwisha, hivyo apulize filimbi ya kumalizia zoezi la kuzunguka uwanja. Si simulizi, ni hali halisi, si hadithi ya kubuni kutoka kwenye kichwa cha mtu, ni ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons